انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧١

وَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِى ٱلرِّزْقِ ۚ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُوا۟ بِرَآدِّى رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَآءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ ٱللَّهِ يَجْحَدُونَ ٧١

{71} Na huu ni katika ushahidi wa upweke wake na ubaya wa kumshirikisha. Yeye Mtukufu anasema kuwa kama vile mnavyoshiriki kwamba nyinyi ni viumbe mnaoruzukiwa, lakini Yeye Mtukufu, "amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki." Kwa hivyo akawafanya miongoni mwenu kuwa huru wenye mali nyingi. Na miongoni mwenu kuna watumwa wao wasiomiliki kitu katika dunia. Kwa hivyo, kama vile mabwana zao, ambao Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha juu yao katika riziki, hawawezi "kurudisha riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo" na wanaona kwamba hili ni katika mambo yasiyowezekana. Basi vile vile wale mliowashirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu, hao kwa hakika ni waja, hawana chochote katika Ufalme uzito wa chembe. Basi vipi mnawafanya kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Je, hii si katika dhuluma kubwa zaidi na kukataa neema za Mwenyezi Mungu? Kwa hivyo, ndiyo maana akasema, "Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?" Kwa hivyo, ikiwa wangekiri neema hizo na wakazinasibisha na yule aliyewapa kuzisimamia, basi wasingemshirikisha na yeyote.