النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمْ ۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرْذَلِ ٱلْعُمُرِ لِكَىْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ ٧٠
{70} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba yeye ndiye aliyeumba waja wake na akawahamisha katika uumbaji awamu baada ya awamu. Kisha baada ya kukamilisha muda wao, anawafisha. Na kuna wengine wao anawapa umri mrefu mpaka akarudishwa "kwenye umri mbaya kabisa." Yaani, umri duni zaidi, ambao kwa huo mtu anafikia udhaifu wa nguvu za dhahiri na za ndani, mpaka akili ambayo ndiyo kiini cha mtu inazidi kuwa dhaifu, hivi kwamba anasahau kile alichokuwa anakijua, na akili yake inakuwa kama akili ya mtoto. Na ndiyo sababu akasema, " hata akawa hajui kitu baada ya kuwa alikuwa anajua. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi, Muweza." yaani elimu yake na uwezo wake vimezunguka vitu vyote. Na katika hayo ni yale anayohamishwa kwayo mwanadamu kutoka awamu za kuumbwa kwake uumbaji mmoja hadi uumbaji mwingine, kama alivyosema Yeye Mtukufu, " Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba kutokana na udhaifu, kisha akajaalia nguvu baada ya udhaifu, kisha akajaalia baada ya nguvu udhaifu tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye ajuaye zaidi, Mwenye uwezo zaidi."