انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٠

فَلَمَّا ٱسْتَيْـَٔسُوا۟ مِنْهُ خَلَصُوا۟ نَجِيًّا ۖ قَالَ كَبِيرُهُمْ أَلَمْ تَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ أَبَاكُمْ قَدْ أَخَذَ عَلَيْكُم مَّوْثِقًا مِّنَ ٱللَّهِ وَمِن قَبْلُ مَا فَرَّطتُمْ فِى يُوسُفَ ۖ فَلَنْ أَبْرَحَ ٱلْأَرْضَ حَتَّىٰ يَأْذَنَ لِىٓ أَبِىٓ أَوْ يَحْكُمَ ٱللَّهُ لِى ۖ وَهُوَ خَيْرُ ٱلْحَـٰكِمِينَ ٨٠

{80} Yaani, ndugu zake Yusuf walipokata tamaa juu ya Yusuf kuwaruhusu kumchukua ndugu yao, “wakaenda kando kunong'ona.” Yaani, walikusanyika peke yao, na hakuna mtu mwingine asliyekuwa pamoja nao, na wakaanza kunong'onezana wao kwa wao. Kisha "Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kutoka kwenu kwa Mwenyezi Mungu” kwamba mtamlinda na kwamba mtakuja naye isipokuwa ikiwa atazungukwa. "Na kabla ya hapo namna mlivyokosa katika agano lenu juu ya Yusuf?” Basi wakawakusanyikia Mambo mawili haya: kutotomiza kwenu agano kulikotangulia kuhusiana na Yusuf, na kushindwa kwenu kumleta ndugu yenu kulikofuata huku. Basi mimi Sina uso nitakaokabiliana nao baba yangu. "Basi mimi sitatoka nchi hii;” yaani, nitakaa katika nchi hii bila ya kuondoka humo, “mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie.” Yaani, aniandikie kuja nyumbani peke yangu au pamoja na ndugu yangu, "Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu.”