انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٨

وَلَمَّا دَخَلُوا۟ مِنْ حَيْثُ أَمَرَهُمْ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغْنِى عَنْهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ إِلَّا حَاجَةً فِى نَفْسِ يَعْقُوبَ قَضَىٰهَا ۚ وَإِنَّهُۥ لَذُو عِلْمٍ لِّمَا عَلَّمْنَـٰهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ٦٨

{68}. “Na” walipokwenda na “wakaingilia pale alipowaamrisha baba yao, hakuwa” kwa kitendo hicho “akiwafaa kitu isipokuwa ni haja tu iliyokuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliyoitimiza.” Na hilo lilimlazimu kwa sababu ya huruma kubwa yake na upendo kwa watoto, kwa hivyo kwa hilo akapata kutulia na kutimiza kile kilicho katika fikira zake. Na huu haukuwa upungufu katika elimu yake. Kwani yeye ni miongoni mwa Mitume watukufu na wenye elimu wanaomuabudu Mwenyezi Mungu tu, na ndiyo maana akasema kumhusu: "Na hakika yeye alikuwa na elimu;” yaani, ana elimu nyingi, "kwa sababu tulimfundisha," na si kutokana na uwezo wake na nguvu yake ndiyo aliyajua hayo. Bali ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na kufundisha kwake. "Lakini wengi wa watu hawajui” mwisho wa mambo na undani wa mambo. Na vile vile wanachuoni miongoni mwao, inafichikana kwao elimu nyingi, na hukumu zake na athari zake.