يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالَ هَلْ ءَامَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَآ أَمِنتُكُمْ عَلَىٰٓ أَخِيهِ مِن قَبْلُ ۖ فَٱللَّهُ خَيْرٌ حَـٰفِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ ٦٤
{64} Yaaqub amani iwe juu yake akawaambia: “Je, niwaamini juu yake isipokuwa kama nilivyowaamini kwa nduguye zamani?” Yaani, mlikwisha tangulia hapo awali kuweka ahadi kubwa kuliko hii kuhusiana na kumhifadhi Yusuf, lakini pamoja na hayo, hamkutimiza yale mliyofunga ahadi nayo kwa msisitizo, kwa hivyo siamini ahadi yenu na ulinzi wenu, lakini ninamwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi wa kulinda, naye ndiye Mbora zaidi wa wanaorehemu.” Yaani, anaijua hali yangu na nataraji kwamba atanirehemu, hivyo atamlinda na kumrudisha kwangu. Na ni kana kwamba kwa maneno haya alikuwa ameshakubali kumuachilia akwende pamoja nao.