انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣١

فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَـًٔا وَءَاتَتْ كُلَّ وَٰحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ ٱخْرُجْ عَلَيْهِنَّ ۖ فَلَمَّا رَأَيْنَهُۥٓ أَكْبَرْنَهُۥ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَـٰشَ لِلَّهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ ٣١

{31} Na kauli hii kwa upande wao ilikuwa ni njama, na haikukusudiwa tu kumlaumu na kumkashifu, bali walitaka, kwa maneno haya, kufikia kumuona huyu Yusuf, ambaye naye mke wa mheshimiwa huyu alifitinishwa naye ili mke wa mheshimiwa huyu akasirike na awaonyeshe ili wamkubalie udhuru wake. Na ndiyo maana wakaiita njama, kwa hivyo akasema: "Basi aliposikia yule bibi masengenyo yao, aliwaita" yaani aliwaita nyumbani kwake kwa ajili ya karamu, "na akawawekea matakia ya kuegemea." Yaani, pahali palipoandaliwa kwa kila aina ya magodoro, mito, na vyakula vitamu. Na miongoni mwa vitu alivyoleta katika karamu hiyo ni chakula kilichohitaji kisu. Ima tunda la utruj au kitu kinginecho. "Na akampa kila mmoja wao kisu" ili wakate kwacho chakula hicho, "na akamwambia" Yusuf, "Tokeza mbele yao," katika hali ya uzuri wake na urembo wake. "Basi walipomwona, waliona ni kitu kikubwa kabisa" katika vifua vyao na wakaona mandhari ya ajabu mno ambayo hawakuwahi kuona mfano wake. "Na wakajikatakata mikono yao" kwa sababu ya mshango kwa visu hivyo walivyokuwa navyo. "Wakasema: Hasha Lillahi!' Yaani, wakamtakasa Mwenyezi Mungu, "Huyu si mwanadamu. Huyu si isipokuwa Malaika mtukufu." Na hayo ni kwa sababu Yusuf alipewa uzuri wa ajabu mno, na nuru na urembo ambayo kwayo alikuwa ni ishara kwa watazamaji na mazingatia kwa wanaotafakari.