يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالَ نِسْوَةٌ فِى ٱلْمَدِينَةِ ٱمْرَأَتُ ٱلْعَزِيزِ تُرَٰوِدُ فَتَىٰهَا عَن نَّفْسِهِۦ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَىٰهَا فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ ٣٠
{30} Inamaanisha kwamba habari hiyo ikawa maarufu na kuenea katika nchi, na wanawake wakazungumza juu yake, na wakaanza kumlaumu mwanamke wa mheshimiwa huyu na wanasema: "Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake bila ya yeye kumtaka! Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni." Yaani, hili ni jambo baya! Yeye ni mwanamke wa cheo kikubwa, na mumewe ni wa cheo kikubwa pia, lakini pamoja na hayo hajaacha kuendelea kumtaka kimapenzi mtumishi wake ambaye yuko chini ya mkono wake na katika huduma yake bila ya yeye kumtaka kimapenzi, na tena pamoja na hayo kumpenda kwake kumemfika kiwango kikubwa sana. "Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni." Yaani, mapenzi yake yamemfika ndani kabisa ya moyo wake. Na huu ndio upendo mkubwa zaidi unaowezekana. "Sisi hakika tunamwona yumo katika upotovu ulio dhahiri." Kwa kuwa ilipatikana ndani yake hali hii ambayo haimfailii, ambayo ni hali inayomshushia hadhi yake na kumdunisha mbele ya watu.