هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالُوا۟ يَـٰنُوحُ قَدْ جَـٰدَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَٰلَنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ ٣٢
{32} Basi walipomuona hayaachi yale aliyokuwa juu yake ya kuwalingania na hawakupata walichotaka kutoka kwake, "Wakasema: Ewe Nuhu! Umejadiliana nasi, na umekithirisha kutujadili. Basi tuletee hayo unayotuahidi" [ya adhabu], "ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli." Lakini ni wajinga kiasi gani hiki, na ni wapotofu kiasi gani hiki wawalipomwambia Mtume wao, mshauri mwaminifu maneno haya! Kwa nini hawakusema ikiwa wao ni wakweli: Ewe Nuhu! Umetunasihi, na umetuonea huruma sana, na umetulingania kwa jambo ambalo halijakuwa wazi kwetu, kwa hivyo tunataka utufafanulie ili tukufuate, vinginevyo basi tunakushukuru kwa ushauri wako. Basi hili lingelikuwa ni jibu la uadilifu kwa yule aliyeitwa kufanya jambo lililofichika kwake, lakini wao katika hayo waliyoyasema walikuwa waongo, na wakawa wamemfanyia ujasiri Nabii wao. Na wala hawakukataa yale aliyoyasema kwa sababu ya shaka hata iliyo kidogo zaidi, achilia mbali kwamba wayakatee kwa hoja. Na ndiyo maana wakapinda kwa ujinga wao na dhuluma yao kwenda kujiharakishia adhabu na kumuona Mwenyezi Mungu kwamba hawezi.