انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · هود
السورة ١١

هود

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣١

وَلَآ أَقُولُ لَكُمْ عِندِى خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعْلَمُ ٱلْغَيْبَ وَلَآ أَقُولُ إِنِّى مَلَكٌ وَلَآ أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِىٓ أَعْيُنُكُمْ لَن يُؤْتِيَهُمُ ٱللَّهُ خَيْرًا ۖ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا فِىٓ أَنفُسِهِمْ ۖ إِنِّىٓ إِذًا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ٣١

{31} "Wala siwaambii kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa mimi ninajua mambo ya ghaibu, wala sisemi: Mimi ni Malaika." Yaani, Mwisho wangu ni kuwa mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Ninawabashiria na ninawaonya, na mengine yasiyokuwa hayo, basi hakuna chochote katika hayo mkononi mwangu. Kwa maana sina hazina za Mwenyezi Mungu, ili niweze kuziendesha, na nimpe nimtakaye, na nimnyime nimtakaye. "Wala mimi sijui mambo ya ghaibu" ili nawajulishe siri zenu na mambo ya ndani yenu. "Wala sisemi Mimi ni Malaika." Maana yake ni kuwa sidai cheo juu ya cheo changu, wala daraja isiyokuwa ile daraja ambayo Mwenyezi Mungu aliniteremsha hapo, wala mimi siwahukumu watu kwa dhana yangu tu. Kwa hivyo, "Wala sisemi kuhusu wale ambao yanawadharau macho yenu." Yaani, Waumini wanyonge ambao wanadharauliwa na wakuu hao waliokufuru; "kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa heri. Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi yaliyo katika nafsi zao." Kwa hivyo, ikiwa wao ni wakweli katika imani yao, basi wana heri nyingi. Na kama wao si hivyo, basi Hesabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu. "Mimi Hapo bila ya shaka;" yaani, ikiwa nitawaambia kitu katika hayo yaliyotangulia "nitakuwa miongoni mwa madhalimu." Na hili ni kuwakatisha tamaa - yeye rehema na amani za mwenyezi mungu ziwe juu yake, - kaumu yake kuwafukuza Waumini maskini, au kuwachukia na kuwashawishi kaumu yake wa njia za kushawishi kwa yule ambaye ni mwadilifu.