هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا تَرْكَنُوٓا۟ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنْ أَوْلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ١١٣
{113} Na ndiyo maana akawatahadharisha dhidi ya kuelekea upande wa wale waliopindukia unyoofu, kwa hivyo akasema: "Wala msiwategemee" [Yaani msielekee upande wa] "wale waliodhulumu." Kwani, mkielekea upande wao na mkakubaliana nao katika dhuluma yao au mkaridhia dhuluma wafanyayo hiyo, basi "mkaja kuguswa na Moto" mkifanya hivyo. "Wala nyinyi hamna walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu" watakaowakinga kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hawatawapatia chochote katika malipo ya Mwenyezi Mungu. "Wala tena hamtanusuriwa;" yaani, hakuna atakayewazuilia adhabu itakapowagusa. Basi katika Aya hii, kuna tahadharisho dhidi ya kumtegemea kila dhalimu. Na maana ya kuegemea ni kuelekea upande wake na kuungana naye katika dhuluma yake na kukubaliana naye katika hilo na kuridhia dhuluma hiyo anayofanya. Na ikiwa ahadi hii ya adhabu ni kuhusiana na kuwaelekea madhalimu, basi vipi hali ya madhalimu wenyewe? Tunamuomba Mwenyezi Mungu salama kutokana na dhuluma.