هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَٱسْتَقِمْ كَمَآ أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا۟ ۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ١١٢
{112} Kisha alipojulisha kuhusu kutonyooka kwao ambako kuliwasababishia kutofautiana na kutengana, akamuamrisha Nabii wake Muhammad - rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na wale walio pamoja naye miongoni mwa Waumini kwamba wanyooke kama walivyoamrishwa, kwa kufuata sheria alizoziweka Mwenyezi Mungu, na waitakidi yale aliyojulisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa itikaki mbalimbali sahihi, wala wasikengeuke wakaacha hayo kwenda kulia wala kushoto, na kwamba wadumu hivyo, wala wasivuke mipaka ya unyoofu aliyowawekea Mwenyezi Mungu. Na kauli yake: "Hakika Yeye anayaona yote myatendayo." Yaani, hakifichiki kwake chochote katika matendo yenu, na atawalipa kwa hayo; basi ndani yake kuna himizo juu ya kufuata unyoofu na kuhofisha dhidi ya kufuata kinyume chake.