الكوثر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنْحَرْ ٢
{2} Na alipomtajia wema wake juu yake; akamuamrisha kumshukuru, akasema: "Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi." Amezitaja ibada hizi mbili hasa kwa sababu hizo ndizo ibada bora kabisa na mambo matukufu zaidi ya kujiweka kwayo karibu na Mwenyezi Mungu, na kwa sababu swala inajumuisha kunyenyekea moyoni na kwa viungo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na humhamisha kupitia aina mbali mbali za uja. Na katika kuchinja kuna kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa bora zaidi alicho nacho mja miongoni mwa dhabihu, na kutoa mali ambazo roho zimefanywa kuzipenda na kuzifanyia ubahili.