انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٣

وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِى ٱلْعُمْىَ وَلَوْ كَانُوا۟ لَا يُبْصِرُونَ ٤٣

{43} Kisha akataja kufungika kwa njia ya pili, ambayo ni njia ya kutazama, akasema: "Na miongoni mwao kuna yule anayekutazama” lakini hakumnufaishi kitu kukutazama kwake, wala hakuzichunguza vyema hali zako. Kwa hivyo, kama vile usivyoweza kuwaongoa vipofu hata kama hawaoni, basi vile vile huwezi kuwaongoa watu hawa. Ikiwa akili zao, na kusikia kwao, na kuona kwao ambazo ndizo njia zinazofikisha kwenye kujua haki, basi iwapi njia ya kuwafikisha kwenye haki? Na ilionyesha kauli yake: "Na miongoni mwao kuna yule anayekutazama” hadi mwisho wa Aya ... kuwa kutazama hali ya Nabii - rehema na Amani za Mwenyezi mungu zimshukie - na mwongozo wake, na maadili yake, matendo yake, na anachokilingania ni katika ushahidi mkubwa zaidi juu ya ukweli wake na usahihi wa kile alichokuja nacho, na kwamba inamtosha mwenye utambuzi bila ya kuhitaji ushahidi mwingine.