يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ ٱلصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا۟ لَا يَعْقِلُونَ ٤٢
{42} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu baadhi ya waliomkadhibisha Mtume, na yale aliyokuja nayo: "Na" hakika “miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza” ewe Nabii - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - wakati unaposoma ufunuo, si kwa sababu ya kutaka kuongoka, bali ni kwa njia ya kufurahia tu, na kukadhibisha, na kutafuta makosa. Na kusikiliza huku si kwa kunufaisha wala si kwa kuwaletea watu wake heri yoyote. Na hakuna shaka kwamba ndiyo maana ukafungika kwao mlango wa mafanikio, na wakanyimwa katika faida ya kusikiliza. Na ndiyo maana akasema, “Je, wewe unaweza wasikizisha viziwi hata kama hawatumii akili?” Na mbinu hii ya kuuliza ni ile yenye maana ya kukanusha na kuthibitisha hilo. Yaani, huwezi kuwasikizisha viziwi ambao hawawezi kusikia kauli hata ukaisema kwa sauti kubwa, hasa ikiwa akili zao hazipo. Kwa hivyo, ikiwa haiwezekani kumsikizisha kiziwi ambaye haelewi maneno, basi wakadhibishaji hawa vile vile haiwezekani kwako kuwaskizisha kusikia ambako watanufaika nako. Ama kusikia hoja, basi hakika walikwisha yasikia yale yanayosimamisha hoja ya kukata ya Mwenyezi Mungu. Basi hii hapa njia kubwa miongoni mwa njia za kutafuta elimu tayari imejifunga kwao, ambayo ni njia ya yanayosikika ambayo yanahusiana na habari.