يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَـٰنَ ٱلضُّرُّ دَعَانَا لِجَنۢبِهِۦٓ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَآئِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُۥ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَآ إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُۥ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ١٢
{12} Na huku ni kujulisha kuhusu umbile la mwanadamu namna alivyo, kwamba yanapomgusa madhara kama vile maradhi au msiba, ataomba dua kwa bidii, na kumwomba mwenyezi Mungu katika hali zake zote huku amesimama, na kuketi, na kulala chini, na atasisitiza katika dua yake hiyo ili Mwenyezi Mungu amwondolee madhara yake. "Lakini tunapomwondoshea shida yake hiyo, huendelea kama kwamba hakuwahi kutuomba tumwondoshee shida iliyomgusa.” Yaani, anaendelea kughafilika huku amempa mgongo Mola wake Mlezi, kana kwamba hakujiwa na madhara yoyote, na Mwenyezi Mungu akamuondolea. Basi Je, ni dhuluma gani iliyo kubwa zaidi kuliko dhuluma hii? Anamwomba Mwenyezi Mungu atimize kusudio lake. Basi anapompa hilo kusudio lake, haitazami haki ya Mola wake Mlezi, kana kwamba hakuna haki yoyote ya Mwenyezi Mungu juu yake? Na huku ni kupambiwa na Shetani. Alimpambia yale ambayo ni ya kuchukiza na yaliyo mabaya katika akili na maumbile. "Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapitilizao viwango yale waliyokuwa wakiyatenda.”