يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَوْ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسْتِعْجَالَهُم بِٱلْخَيْرِ لَقُضِىَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا فِى طُغْيَـٰنِهِمْ يَعْمَهُونَ ١١
{11} Na hili ni katika upole wake na wema wake kwa waja wake, kwamba ikiwa angewaharakishia maovu wanapofanya sababu zake, na akawaharakishia adhabu juu yake kama anavyowaharakishia heri wanapofanya sababu zake, “basi bila ya shaka wangelikwisha timiziwa muda wao.” Yaani, adhabu ingewafutilia mbali. Lakini Yeye Mtukufu anawapa muhula wala hawapuuzi, na anasamehe nyingi katika haki zake. Basi lau kuwa Mwenyezi Mungu angewaadhibu watu kwa mujibu wa dhuluma zao, basi asingelimwacha mnyama yeyote juu ya mgongo wake. Na inaingia katika hili kwamba mja anapowakasirikia watoto wake, au mkwe, mali yake, basi huenda akawaapiza kuapiza ambako lau kutakubaliwa wangeangamia na hilo lingelimdhuru kumdhuru kukubwa sana, lakini Yeye Mtukufu ni Mpole, Mwenye hekima. Na kauli yake: "Lakini tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi;” yaani, wasioamini Akhera. Na kwa sababu ya hilo, hawajitayarishi kwa ajili yake wala hawafanyi yenye kuwaepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu, "katika upotovu wao.” Yaani, batili yao ambayo walivuka kwayo haki na mipaka “wakihangaika;” yaani, wanasitasita na kuchanganyikiwa bila ya kuongoka kwenye njia ya sawa, wala hawawezeshwi kufikia hoja iliyo imara. Na hiyo ni adhabu kwao kwa dhuluma yao na kukufuru kwao ishara za Mwenyezi Mungu.