سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورت 9

At-Tawba

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 29

قَـٰتِلُوا۟ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ ٱلْحَقِّ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ حَتَّىٰ يُعْطُوا۟ ٱلْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَـٰغِرُونَ 29

{29} Aya hii ni amri ya kupigana vita na makafiri miongoni mwa Mayahudi na Wakristo miongoni mwa "wale wasiomuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho" imani sahihi ambayo wanaisadikisha kwa vitendo yao na matendo yao, "wala hawaharamishi yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, hawaifuati sheria Yake katika kuharamisha vitu vilivyoharamishwa, "wala hawashiki Dini ya haki" yaani, hawashiki Dini sahihi, hata kama watadai kwamba wako katika dini, lakini hiyo ni dini isiyokuwa ya haki. Kwa sababu ima ni dini iliyobadilishwa, nao ni ile ambayo Mwenyezi Mungu kamwe hakuiamrisha, na ima ni dini iliyofutiliwa mbali, ambayo Mwenyezi Mungu aliiamrisha hapo awali kisha akaibadilisha kwa sheria ya Muhammad - rehema na amani za mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa hivyo ikabakia kwamba kushikamana nayo baada kufutiliwa kwake hakuruhusiki. Basi amri yake ya kupigana na hawa, na akahimiza juu ya hilo kwa sababu wanalingania kwa yale waliyo juu yake, na yanatokea madhara mengi juu ya watu kutoka kwao, kwa sababu wao ni watu wa Kitabu. Na aliviwekea muda vita hivyo "mpaka watoe kodi;" yaani, mali ambayo ni malipo kwa Waislamu kuacha kupigana nao, na kuwaacha wakae kwa amani juu ya nafsi zao, na mali zao miongoni mwa Waislamu. Inachukuliwa kutoka kwao kila mwaka, kila mmoja kulingana na hali yake, miongoni mwa tajiri na maskini, na wa wastani, kama alivyofanya hivyo amiri wa Waumini, Umar Ibn Al-Khattab na wengineo miongoni mwa maamiri wa Waumini. Na kauli yake, "kwa hiari yao;" yaani, mpaka waitoe huku wamefedheheka bila ya kuwa na uwezo, na waitoe kwa mikono yao, wala wasimtume mtumishi wao nayo wala asiyekuwa wao. Bali haikubaliki isipokuwa kutoka katika mikono yao, "hali wametii." Kwa hivyo, watakapokuwa katika hali hii, na wakawaomba Waislamu kwamba wawakubalie kutoa jizya (kodi) hiyo hali ya kuwa wako chini ya hukumu za Waislamu na utawala wao, na katika hali ya kuwa salama kutokana na uovu wao, na fitina zao, na wakajisalimisha kwa masharti ambayo Waislamu waliyaweka juu yao, miongoni mwa yale yanayozuia utukufu wao na kiburi chao, na yanasababisha kufedheheka kwao na kudunika kwao, basi inakuwa wajibu kwa imam au naibu wake kwamba afanye mapatano hayo nao. Lakini ikiwa ni kwamba hawatatimiza, wala hawatatoa jizyah kwa hiari yao hali ya kuwa wametii, basi haitaruhusiwa kuwakubalia kutoa jizya, lakini watapigwa vita hadi wasilimu. Na walitumia Aya hii kama ushahidi wengi wa wanazuoni wanaosema kwamba Jizyah (kodi) haichukuliwi isipokuwa kutoka kwa Watu wa Kitabu, kwa sababu Mwenyezi Mungu hakutaja kuchukua jizyah isipokuwa kutoka kwao, na ama wasiokuwa wao, hao hakutaja isipokuwa kupigana vita nao mpaka wasilimu. Na Majusi walifungamanishwa na Watu wa Kitabu kuhusiana na kuchukua jizyah na kuwakubalia kukaa katika nchi ya Waisilamu. Kwa maana Nabii rehema na amani za Allah zimshukie alichukua jizyah kutoka kwa Majusi wa Hajar, kisha amiri wa Waumini, 'Umar pia akaichukua kutoka Waajemi ambao walikuwa Majusi. Na ilisemwa kuwa Jizyah inachukuliwa kutoka kwa makafiri wote kama vile Watu wa Kitabu na wengineo, kwa sababu aya hii iliteremka baada ya kukamilika kwa kupigana vita na Waarabu washirikina na kuanza kupigana vita na Watu wa Kitabu na mfano wao. Kwa hivyo kunakuwa kufungia huku ni ripoti tu juu ya hali halisi, na haina maana ya kinyume. Na hilo linaonyeshwa kwa sababu Majusi ilichukuliwa jizyah kutoka kwao nao sio katika Watu wa Kitabu, na kwa sababu imeripotiwa kwa habari nyingi sahihi kutoka kwa Waislamu miongoni mwa Maswahaba na wale wa baada yao kwamba walikuwa wakiwaita wale wanaopigana nao kwa moja ya matatu: Ima kusilimu, au kulipa jizya, au upanga, bila ya kutofautisha kati ya mtu wa kitabu na wengineo.