At-Tawba
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ ۗ وَيَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ 15
{15} "Na aondoe hasira ya nyoyo zao," kwani katika nyoyo zao kuna chuki na hasira dhidi yao, ambayo kupigana nao na kuwaua kwao ni poza ya yale yaliyo katika nyoyo za Waumini ya huzuni na wasiwasi; kwa kuwa, wanawaona maadui hawa wanampiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na wanajitahidi katika kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu, na kuondoa hasira iliyo katika nyoyo zenu. Na hili linaonyesha upendo wa Mwenyezi Mungu kwa waumini, na kuzitunza kwake hali zao, kiasi kwamba alifanya katika jumla ya madhumuni ya kisheria ni kuponya yale yaliyo ndani ya mioyo yao na kuiondoa hasira yao. Kisha akasema: "Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba amtakaye" miongoni mwa wapiganaji hawa, kwa kuwawezesha kuingia katika Uislamu, na kuupamba katika nyoyo zao, na kuwachukizia ukafiri, na uvukaji wa mipaka, na uasi. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima kubwa." Yeye huweka vitu pahali pake, na anajua ni nani anayeifailia imani, kwa hivyo anamwongoa, na yule asiyeifailia, kwa hivyo anambakisha katika upotofu wake na upindukiaji wake mipaka.