At-Tawba
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَمَا كَانَ ٱلْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا۟ كَآفَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَآئِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا۟ فِى ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُوا۟ قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوٓا۟ إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ 122
{122} Yeye Mtukufu anasema akiwabainishia waja wake Waumini yale yanayowapasa "Na haiwapasi Waumini kutoka wote pamoja." Yaani, wote kwa pamoja ili kupigana na adui yao. Kwa maana, hilo litawasababishia magumu, na yatapotea kwalo manufaa mengine mengi. "Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao?” Yaani, kutoka katika nchi, makabila, na makabila madogo ambao watatosheleza na kufikia makusudio, basi ingekuwa bora zaidi. Kisha akatanabahisha kwamba, kuna masilahi katika kukaa kwa wale wanaokaa miongoni mwao na kutotoka kwao ambayo ikiwa wangetoka wangeyakosa, akasema: "wakajifunze vyema.” Yaani, wale wanaokaa nyuma katika "Dini kisha waje kuwaonya wenzao watakapowarudia.” Yaani, wajifunze elimu ya kisheria, na kujua maana zake, na waelewe siri zake, na wawafundishe wengine, na wawaonye kaumu yao watakapowarudia. Basi katika hili kuna fadhila ya elimu, hasa kuifahamu sheria ya dini, na kwamba ndiyo jambo muhimu zaidi, na kwamba mwenye kujifunza elimu, ni inamlazimu aieneze na kuitawanya kwa waja na kuwashauri ndani yake. Kwa maana kuenea elimu kutoka kwa mwanachuoni ni katika baraka zake na malipo yake yanayokuwa. Na ama mwanachuoni kujibakishia yeye mwenyewe elimu bila ya kulingania katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa hekima na mawaidha mazuri, na kuacha kuwafundisha wasiojuwa wanayofaa kufanya, basi Waislamu watapata manufaa gani kutokana kwake? Na mwisho wake ni yeye mwenyewe kufa, kwa hivyo; ikafa elimu yake hiyo na matunda yake, na hili ndiko kunyimwa kukubwa mno kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alimpa elimu na akampa ufahamu. Na katika Aya hii pia kuna ushahidi, mwongozo, na tanabahisho muhimu sana juu ya faida kubwa, ambayo ni kwamba Waislamu wanapaswa wamwandae mtu atakayetekeleza masilahi miongoni mwa masilahi ya umma, na aliwekee hilo wakati wake mwingi, na alifanyie bidii, na asitazame lisilokuwa hilo, ili masilahi yao yasimame sawasawa, na manufaa yao yatimie, na ili uwe mwelekeo wao wote na mwisho wao wanaoukusudia ni kusudio moja. Nao ni kusimamisha masilahi ya dini yao na dunia yao, hata kama njia zitagawanyika na mbinu zikawa mbalimbali. Kwani matendo yanawezakuwa tofauti, lakini kusudio ni moja. Na hii ni katika hekima ya ujumla yenye manufaa katika mambo yote.