At-Tawba
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
ٱلتَّـٰٓئِبُونَ ٱلْعَـٰبِدُونَ ٱلْحَـٰمِدُونَ ٱلسَّـٰٓئِحُونَ ٱلرَّٰكِعُونَ ٱلسَّـٰجِدُونَ ٱلْـَٔامِرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَٱلنَّاهُونَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَٱلْحَـٰفِظُونَ لِحُدُودِ ٱللَّهِ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ 112
{112} Ni kana kwamba ilisemwa: Ni nani hao Waumini ambao wana bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba wataingia Peponi na kupata utukufu? Akasema: “Wale wanaotubia;” yaani, wale wanaoshikamana na toba katika kila wakati juu ya mabaya yote. "Wanaoabudu;” yaani, wale ambao wana sifa ya uja kwa Mwenyezi Mungu na kuendelea kumtii kwa kutekeleza wajibu mbalimbali na matendo yanayopendekenzwa katika kila wakati, na kwa hayo anakuwa mja miongoni mwa wanaoabudu. “Wanaomhimidi” Mwenyezi Mungu katika nyakati za heri, nyakati mbaya, katika wepesi na dhiki, wale wanaozikiri neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yao, za wazi na zilizofichika, na wanamsifu Mwenyezi Mungu kwa kuzitaja, na kumtaja katika nyakati za usiku na mchana. "Wanaokimbilia heri;” yaani, wanaofunga saumu, au wale wanaosafiri kwa ajili ya kutafuta elimu. Na pia ilitafsiriwa kwamba maana yake ni moyo kuingia katika kumjua Mwenyezi Mungu, na kumpenda, na kumrudia Yeye daima. Na maana sahihi yake ni kusafiri kwa ajili ya kwenda kufanya mambo ya kujikurubisha nao kwa Mwenyezi Mungu, kama vile Hijja, na Umra, na Jihad, na kutafuta elimu, na kuwaunga jamaa na mfano wake. "Wanaorukuu, wanaosujudu;” yaani, wanaoswali kwa wingi, ambalo linajumuisha kurukuu na kusujudu. “Wanaoamrisha mema;” na zinaingia katika hilo wajibu zote. "Na wanaokataza maovu;" nayo ni yote aliyoyakataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake. "Na wanaolinda mipaka ya Mwenyezi Mungu” kwa kujifunza mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake, na yale yanayoingia katika maamrisho, na makatazo, na hukumu mbalimbali, na yale yasiyoingia ndani yake, wale wanaodumu kwayo kwa kufanya na kuacha na kutokuwepo. "Na wabashirie Waumini." Hakutaja kile wanachobashiria ili yaingie humo yale yote yaliyofungamanishwa na imani miongoni mwa thawabu za dunia hii, na dini, na akhera. Na bishara hiyo inamjumuisha kila Muumini. Lakini kiwango chake na sifa yake, basi hayo ni kulingana na hali ya waumini na imani yao, kinguvu na kiudhaifu wao, na kwa kutenda ipasavyo.