Al-Jumu'a
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَإِذَا رَأَوْا۟ تِجَـٰرَةً أَوْ لَهْوًا ٱنفَضُّوٓا۟ إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌ مِّنَ ٱللَّهْوِ وَمِنَ ٱلتِّجَـٰرَةِ ۚ وَٱللَّهُ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ 11
{11} "Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo." Yaani wanatoka msikitini kwa kutafuta kwa bidii pumbao hilo na biashara hiyo, na wakaacha heri, "na wakakuacha umesimama" ukihutubia watu. Hilo lilikuwa siku ya Ijumaa, wakati Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipokuwa anahutubia watu, tazama, ukaja msafara wa kibiashara Madina. Watu waliposikia juu yake ilhali wapo msikitini, wakatawanyika kutoka msikitini na wakamwacha Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akitoa khutba, wakiharakishia kile kisichofaa kuharakishiwa, na kuacha adabu nzuri. "Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu" ya malipo mazuri kwa anayedumu katika heri na akajisubirisha katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, "ni bora kuliko pumbao na biashara" ambayo ingawa makusudio machache yanaweza kutokea humo, lakini hayo ni machache na ya kuisha, na ya kukosesha heri ya Akhera, nayo subira juu ya kumtii Mwenyezi Mungu haikoseshi riziki. "Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki." Kwa hivyo, mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, anamruzuku kutokea pale asipotarajia.
Kuna faida nyingi katika aya hizi: Miongoni mwake ni kwamba swala ya Siku ya Ijumaa ni wajibu kwa Waumini [wote] na wanalazimuka kuifanyia hima, kuiharakishia na kuijali sana. Miongoni mwake ni kwamba khutba mbili za siku ya Ijumaa ni wajibu na lazima zihudhuriwe. Kwa sababu alielezea ukumbusho hapa kwa hotuba hizo mbili, na Mwenyezi Mungu akaamuru kwamba kuziendea na kuzifanyia hima kwa haraka. Miongoni mwake ni kwamba ni katika sheria kuadhini kwa ajili ya Sala ya Ijumaa na kwamba hilo limeamrishwa. Miongoni mwake ni kukataza kununua na kuuza baada ya adhana ya Ijumaa na kuharamisha hayo. Na hilo si isipokuwa kwa sababu yanakosesha faradhi na kujishughulisha mbali nayo. Basi hilo likaashiria kwamba kila jambo hata kama linaruhusika katika asili yake, ikiwa linasababisha kupoteza jambo la wajibu, basi haliruhusiki katika hali hiyo. Miongoni mwake ni amri ya kuhudhuria khutba mbili za siku ya Ijumaa, na kumkashifu asiyezihudhuria, na inamlazimu mwenye kuzihudhuria kuzisikiliza kwa utulivu. Miongoni mwake ni kwamba mja ambaye anakaribia kumwabudu Mwenyezi Mungu wakati ambapo nafsi yake inamuita kwenye mambo ya pumbao, biashara na matamanio, anapaswa kuikumbusha mambo mema aliyo nayo Mwenyezi Mungu na kuipendelea radhi ya Mwenyezi Mungu kuliko matamanio yake.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Jumu'a kwa neema na msaada Mwenyezi Mungu. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.