Al-An'aam
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَلِكُلٍّ دَرَجَـٰتٌ مِّمَّا عَمِلُوا۟ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ 132
{132} Lakini hata kama wanashiriki katika hasara, Wao hakika wanatofautiana katika kiasi chake kutofautiana kukubwa. "Na kila mmoja" wao "ana daraja mbalimbali kutokana na yale waliyoyatenda" kulingana na vitendo vyao, hachukuliwi wa ubaya mdogo miongoni mwao kama wa ubaya mwingi wao, wala mfuasi kama aliyefuatwa, wala anayeongozwa kama kiongozi. Kama vile wale wa thawabu na Pepo hata wakishirikiana katika faida, na kufaulu, na kuingia Peponi, lakini kati yao kuna tofauti ambayo haijui isipokuwa Mwenyezi Mungu tu, pamoja na kwamba wote walikwisha ridhia yale aliyowapa Mola wao na wakatosheka na yale aliyowapa bila ya malipo. Basi tunamuomba Mola Mtukufu atujaalie kuwa miongoni mwa wale watakaokuwa katika Firdaws ya juu kabisa, ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia wale walio karibu miongoni mwa waja Wake, na wale walioteuliwa miongoni mwa viumbe Wake, na wale wa juu zaidi miongoni mwa wale anaowapenda. "Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda." Basi atamlipa kila mmoja kulingana na matendo yake, na kwa yale anayoyajua katika makusudio yake.