Al-An'aam
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
لَّا تُدْرِكُهُ ٱلْأَبْصَـٰرُ وَهُوَ يُدْرِكُ ٱلْأَبْصَـٰرَ ۖ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلْخَبِيرُ 103
{103} "Hazungukwi na macho," kwa sababu ya ukuu wake, na taadhima yake, na ukamilifu wake; yaani, macho hayamzunguki, hata ingawa yanamwona na kufurahi kwa kuutazama uso wake mtukufu. Kwa hivyo kukanusha kuzunguka hakukanushi kuona; bali kunauthibitisha kuona kulingana na maana isiyokuwa ya moja kwa moja. Kwani ikiwa anakanusha kuzunguka ambako ni maalumu zaidi katika sifa za kuona, hilo linaonyesha kwamba kuona kumethibiti. Kwa maana ikiwa angetaka kukanusha kuona Angesema: ‘Macho hayamuoni ...’ na mfano wa hilo. Basi ikajulikana kwamba hakuna hoja katika Aya ya dhehebu la Mu’atwila, ambao wanakanusha kumuona Mola wao Mlezi katika Akhera. Bali ndani yake kuna ushahidi kinyume cha kauli yao. "Naye anayazunguka macho," yaani, Yeye ndiye ambaye elimu yake imekizunguka kilicho dhahiri na kilichofichika, na kusikia kwake kumezunguka sauti zote za dhahiri na zilizofichika, na kuona kwake yamekizunguka kila kinachoonekana, kidogo chake na kikubwa chake. Na ndiyo maana akasema, "Naye ni Mjua siri, Mwenye habari zote." Yaani, Yule ambaye elimu yake na kuwa kwake na habari ni kubwa sana na kwa makini kiasi kwamba anazizunguka siri, na yaliyofichika, na ya ndani. Na katika kujua kwake siri, ni kwamba ampeleka mja wake kwenye masilahi ya dini yake, na anayafikisha kwake kwa njia ambazo mja hazihisi wala hazifanyii bidii, na anamfikisha kwenye furaha ya milele na kufaulu kwa milele kutokea mahali asipotarajia, kiasi kwamba Yeye anamkadiria Mambo ambayo mja anayachukia na anapata uchungu kwa sababu yake, na anamuomba mwenyezi Mungu ayaondoe. Kwa sababu anajua kwamba dini yake ni yenye kutengenea zaidi, na kwamba ukamilifu wake unategemea juu yake. Basi Ametakasika yule ambaye ni Mjua siri wa atakalo, Mwenye kuwarehemu Waumini.