سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hadid
سورت 57

Al-Hadid

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 20

ٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌۢ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِى ٱلْأَمْوَٰلِ وَٱلْأَوْلَـٰدِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ ٱلْكُفَّارَ نَبَاتُهُۥ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَىٰهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَـٰمًا ۖ وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضْوَٰنٌ ۚ وَمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَآ إِلَّا مَتَـٰعُ ٱلْغُرُورِ 20

{20} Mwenyezi Mungu anajulisha kuhusu uhalisi wa dunia na jinsi ulivyo, na anaelezea madhumuni yake na madhumuni ya wakazi wake, kwamba ni "mchezo na pumbao." Miili huichezea na nyoyo hujifurahisha kwayo, na hili linathibitishwa na yaliyopo na ni ukweli wa wana dunia. Kwani, utawakuta wanapoteza muda wa maisha yao kwa kufanya pumbao za nyoyo zao na kughafilika mbali na suala la kumkumbuka Mwenyezi Mungu na yale yaliyo mbele yao ya ahadi nzuri na vitisho vya kuadhibiwa. Na utawaona wameifanya dini yao kuwa ni mchezo na pumbao. Tofauti na watu ambao wako macho, na wafanyao matendo sana kwa ajili ya akhera. Mioyo yao imejaa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kumjua vyema na upendo. Wameushughulisha wakati wao kwa matendo yanayowaleta karibu na Mwenyezi Mungu, yenye manufaa yanayowahusu wao tu na manufaa yanayowafikia wengine. Na kauli yake: "Na pambo;" yaani, kujipamba kwa mavazi, vyakula, vinywaji, vipando, nyumba, makasri na kutafuta heshima na mengineyo. "Na kujifahirisha baina yenu" kila mmoja akitaka kuwa mshindi katika mambo yake, na kwamba awe ndiye mwenye umashuhuri zaidi katika hali zake "na kushindana kwa wingi wa mali na watoto." Na hili linathibitishwa na kutokea kwake katika wale wanaoipenda dunia na kuridhika nayo. Tofauti na yule aliyeijua dunia na uhakika wake, basi akaifanya kuwa ni njia tu ya kupitia, na hakuifanya kuwa ni mahali pa kukaa na kutulia, kwa hivyo akashindana katika yale yatakayomuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na akachukua njia zitakazomfikisha kwenye makazi ya utukufu wake. Na akimuona mwenye kukithirisha mali na watoto na kushindana naye, yeye anashindana naye katika matendo mema. Kisha akaipigia dunia mfano wa mvua iliyoteremka juu ya ardhi, na ikachanganyika nayo mimea ya ardhi wanayokula kwayo watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilika katika pambo lake, na mimea yake ikawafurahisha wakulima, ambao hawakuangalia wala hawakuwa na hima juu ya kitu kingine isipokuwa dunia, amri ya Mwenyezi Mungu ikaijia na kuiharibu. Kwa hivyo ikanyauka na kukauka, na kurudi katika hali yake ya mwanzo. Ni kana kwamba hakuna kijani kibichi kilichowahi kuota juu yake, na wala haikuwahi kuwa na mwonekano mzuri mno. Basi dunia pia iko hivyo. Wakati ilikuwa iking'aa kwa mwenye kuitafuta na ikawa na mwonekana mzuri; chochote alichotaka katika mambo yake yanayotakwa, anakipata. Na chochote alicholenga kufanya katika mambo yake anakuta milango yake imefunguliwa sawasawa. Lakini tazama, ikapatwa na yale aliyoipangia Mwenyezi Mungu, nayo yakaiondoa mikononi mwake, au yakamwondoa yeye akaiacha. Kwa hivyo, akaondoka humo mikono mitupu; hakuchukua humo chochote isipokuwa sanda tu. Basi ole wake mwenye kuifanya kuwa ndiyo lengo kubwa zaidi analilotamani, basi akaifanyia matendo na juhudi kubwa. Na ama kuifanyia akhera matendo, hilo ndilo lenye kunufaisha na kuhifadhiwa mwenye kuyafanya matendo hayo na yatafuatana na mja huyo milele, na ndiyo maana Mola Mtukufu akasema: "Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi." Yaani, hali ya Akhera haitoki nje ya mambo mawili: Ima adhabu kali katika moto wa Jahannamu na pingu zake, minyororo yake na vitisho vyake vikubwa kwa yule ambaye dunia ilikuwa ndiyo lengo lake kuu. Kwa hivyo akathubutu kumuasi Mwenyezi Mungu, kukanusha ishara za Mwenyezi Mungu, na kukufuru neema za Mwenyezi Mungu. Au msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa maovu, kuondolewa kwa adhabu mbalimbali, kuridhiwa na Mwenyezi Mungu, na makazi ya kuridhiwa na kuridhia, kwa yule anayemruhusu, ambaye aliijua dunia na akaifanyia Akhera juhudi ipasavyo. Yote hayo ndiyo yanaitia mtu kuipa dunia mgongo na kuitaka sana Akhera, na ndiyo maana akasema: "Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu." Hadanganyiki nayo isipokuwa watu wenye akili dhaifu tu, ambao yule mdanganyifu anawadanganya wamkatae Mwenyezi Mungu.