Al-Hadid
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ ٱللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ ٱلْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ ٱلْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَـٰسِقُونَ 16
{16} Alipotaja hali ya Waumini wanaume na Waumini wanawake na wanafiki wanaume na wanafiki wanawake katika Akhera, hayo yakawa katika yale yanayoziitia nyoyo kumnyenyekea Mola wao Mlezi na kuunyenyekea ukuu wake, basi Mwenyezi Mungu akawakemea Waumini kwa kutofanya hivyo, akasema: "Je, wakati haujafika bado kwa wale walioamini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyoteremka?" Yaani, je, haujafika wakati ambao nyoyo zanafaa kulainika na kuunyenyekea ukumbusho wa Mwenyezi Mungu, nayo ni Qur-ani, na kufuata amri zake na makemeo yake na haki iliyoteremka, ambayo alikuja nayo Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Hili ndani yake limo kuwahimiza Waumini kujitahidi kunyenyekea kwa nyoyo zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyoyataremsha ya Kitabu na hekima, na kwamba Muumini akumbuke mawaidha ya kimungu na hukumu za kisheria kila wakati, na wajifanyie hesabu juu yake. “Wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu." Yaani, wasiwe kama wale ambao Mwenyezi Mungu aliwateremshia Kitabu kinachohitaji unyenyekevu wa moyo na utiifu kamili, kisha hawakudumu juu yake, wala hawakukaa imara juu yake. Bali muda uliwawia mrefu, wakaendelea kughafilika, na imani yao ikafifia, na yakini yao ikaisha. "Kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao ni wapotovu." Hayo ni kwa sababu, nyoyo zinahitaji kila wakati kukumbushwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kufanywa kutamka hekima yake, na wala mtu hafai kughafilika mbali na hayo. Kwani hiyo ni sababu ya ugumu wa moyo na ukavu wa jicho.