سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tur
سورت 52

At-Tur

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 15

أَفَسِحْرٌ هَـٰذَآ أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ 15

{15} "Je, huu ni uchawi au hamuoni tu?" Inawezekana kwamba kilichoashiriwa hapa ni Moto na adhabu. Kama linavyoonyeshwa hilo na muktadha wa aya hii. Yaani, walipouona moto na adhabu; waliambiwa haya kwa njia ya kuwafokea: Je, huu ni uchawi ambao hauna uhakika wowote? Basi tayari mmeshauona? Au mlikuwa hamuoni katika dunia? Wala hamkuwa na ufahamu wala elimu. Bali mlikuwa mkilifanyia ujinga jambo hili, na hakuna hoja iliyothibiti juu yenu?! Na jibu la hayo ni kwamba mambo hayo yote mawili hayapo. Ama kuwa kwake uchawi; Basi imeshawadhihirikia kwamba hilo ndiyo haki ya haki zote na ukweli wa ukweli wote unaopingana na uchawi kwa njia zote. Ama kuhusu kwamba hawaoni; basi hakika jambo hili ni kinyume na hivyo, bali hoja ya Mwenyezi Mungu ilithibiti dhidi yao, na Mitume wakawalingania kuamini jambo hilo, na wakasimamisha ushahidi mbalimbali na hoja juu ya hilo mambo yanayolifanya suala hili kuwa ndilo jambo lenye ushidi mkubwa zaidi, lililo wazi kabisa. Inawezekana kwamba yaliyoashiriwa kwa kauli yake Mwenyezi Mungu "Je, huu ni uchawi, au hamwoni tu?" Ni yale aliyokuja nayo Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ya haki iliyo wazi na njia iliyonyooka. Yaani, je, inawezekana kwa mwenye akili timamu kusema juu yake kwamba hayo ni uchawi, ilhali hayo ndiyo kweli kubwa kabisa na uliotukuka zaidi, lakini kwa sababu ya kukosa kwao utambuzi, wakasema waliyoyasema juu yake?