Al-Maaida
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
جَعَلَ ٱللَّهُ ٱلْكَعْبَةَ ٱلْبَيْتَ ٱلْحَرَامَ قِيَـٰمًا لِّلنَّاسِ وَٱلشَّهْرَ ٱلْحَرَامَ وَٱلْهَدْىَ وَٱلْقَلَـٰٓئِدَ ۚ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ وَأَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ 97
{97} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba aliifanya "Al-Kaaba, Nyumba hii Tukufu, kuwa ya kuwakimu watu;" inasimamia dini yao na dunia yao kwa wao kuitukuza. Na kupitia hayo Uislamu wao unakamilika, na kupitia hayo mizigo yao inaondolewa, na kwa sababu ya kuikusudia wanapata vipawa vingi na ihsani nyingi. Na kwa sababu yake, mali zinatumika na hali nzito zinaingiwa kwa ajili yake, na wanakusanyika ndani yake jamii zote za Waislamu kutoka katika kila njia ya mbali. Kwa hivyo wanajuana, na wanatafuta msaada kutoka kwa wao kwa wao, na wanashauriana juu ya masilahi ya umma, na yanajengeka mafungamano baina yao kwa masilahi yao ya Kidini na ya kidunia. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema; "Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya wanyama hoa wa mifugo aliowaruzuku." Na kwa kuwa Nyumba hii ni pahali pa kusimama pa watu, baadhi ya wanachuoni walisema: Hakika Hijja kwenda katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu ni wajibu na kutosheleza katika kila mwaka; na lau kuwa watu wataiacha Hijja, basi kila mwenye uwezo atapata dhambi. Bali lau kuwa watu wataacha kwenda Hijja huko, basi yataondoka yale ambayo ndani yake kuna Nguvu zao, na Qiyama kitasimama. Na kauli yake, "na dhabihu walioletwa Makka kama zawadi, na dhabihu waliofungwa vigwe." Yaani, vile vile, aliwafanya wanyama wa dhabihu na dhabihu waliofungwa vigwe ambazo ndizo aina tukufu zaidi za wanyama wa dhabihu kuwa vya kuwakimu watu, wananufaika kwavyo na wanalipwa juu yake. "Hayo ni ili mjue ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika mbingu na yaliyo katika ardhi, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu." Kwa hivyo, katika elimu yake ni kwamba aliwafanyia Nyumba hii tukufu kwa sababu ya kile anachokijua ya masilahi yenu ya kidini na ya kidunia.