سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
سورت 5

Al-Maaida

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 94

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَيَبْلُوَنَّكُمُ ٱللَّهُ بِشَىْءٍ مِّنَ ٱلصَّيْدِ تَنَالُهُۥٓ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ ٱللَّهُ مَن يَخَافُهُۥ بِٱلْغَيْبِ ۚ فَمَنِ ٱعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٌ 94

{94} Na hii ni katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, kwamba aliwajulisha yale atakayoyafanya kwa hukumu na majaaliwa, ili wamtii na wasonge mbele kwa ufahamu. Na mwenye kuangamia aangamie kwa hoja iliyo wazi, na mwenye kuishi aishi kwa hoja zilizo wazi. Kwa hivyo Yeye Mtukufu akasema, "Enyi mlioamini," hakuna budi Mwenyezi Mungu atajaribu imani yenu; "Hakika Mwenyezi Mungu atawajaribu kwa kitu kidogo katika mawindo." Yaani, kitu ambacho siyo kingi, kwa hivyo litakuwa jaribio jepesi, kama kurahisisha kwake Yeye Mtukufu na upole. Na hao mawindo ambayo Mwenyezi Mungu atawajaribu kwayo; “inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu;” yaani, itaweza kuyawinda Ili yatimie majaribio kwa hilo, sio wale ambao hawawezi kuwindwa kwa mkono wala mkuki. Kwa hivyo majaribio yanakuwa hayana faida. Kisha akataja hekima katika majaribio hayo, kwa hivyo akasema; "Ili Mwenyezi Mungu amjue;" elimu iliyo dhihiri kwa viumbe ambayo inaambatana na thawabu na adhabu, "mwenye kumhofu katika ghaibu;" basi akajizuia na yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyakataza pamoja na kwamba ana nguvu juu yake, na analiweza. Kwa hivyo anamlipa thawabu nyingi, kuliko yule asiyemhofu katika ghaibu, kwa hivyo hayaachi maasia yanayomjia, kwa hivyo anawinda kile alicho na uwezo juu yake. "Kwa hivyo, mwenye kuvuka mipaka" miongoni mwenu baada ya ubainisho huu ambao ulikata hoja na ukaweka wazi njia, "basi ana adhabu chungu." Yaani, yenye kutia uchungu na maumivu, ambayo hawezi kuieleza isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hakuna udhuru kwa mvuka mipaka huyo, na mazingatio yanazingatiwa kwa anayemuogopa kwa ghaibu na kutokuwepo kwa watu pamoja naye. Ama kudhihirisha kumhofu Mwenyezi Mungu mbele ya watu, bali hilo huenda likawa kwa ajili ya kuwahofu watu, kwa hivyo halipwi kwa hilo.