Al-Maaida
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ قَدْ جَآءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ فَتْرَةٍ مِّنَ ٱلرُّسُلِ أَن تَقُولُوا۟ مَا جَآءَنَا مِنۢ بَشِيرٍ وَلَا نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَآءَكُم بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ 19
{19} Yeye Mwenye baraka, Mtukufu anawalingania Watu wa Kitabu kwa sababu ya yale aliyowaneemesha kwayo ya Kitabu chake. Kwamba wamwamini Mtume wake Muhammad -rehema na amani zimshukie, - na wamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye alimtuma kwao "katika wakati usiokuwa na Mitume," na haja kubwa ya kuja kwake. Na hilo ni katika yale yanayoitia kumwamini, na kwamba anawabainishia matakwa yote ya Mwenyezi Mungu na hukumu za kisheria, na kwa hilo, Mwenyezi Mungu akakata hoja zao; ili wasije wakasema, "Hakutujia mbashiri wala mwonyaji. Basi kwa hakika amekwisha wajia mbashiri na mwonyaji." Anayewabashiria thawabu za sasa na za baadaye, na matendo yenye kupelekea katika hilo, na sifa ya wale wanaoyafanya, na anatahadharisha juu ya adhabu ya sasa na ya baadaye, na matendo yanayopelekea hayo, na sifa ya wale wanaoyafanya. "Na Mwenyezi Mungu ana uweza juu ya kila kitu." Vitu vyote vimefuata kwa hiari, na kunyenyekea kwa sababu ya uwezo wake. Kwa hivyo, Hakuna chochote katika hivyo kinachomuwiya kigumu. Na katika uwezo wake, ni kwamba aliwatuma Mitume na akateremsha Vitabu, na kwamba Yeye humlipa mwenye kuwatii, na humuadhibu mwenye kuwaasi.