Al-Ghaafir
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
رَفِيعُ ٱلدَّرَجَـٰتِ ذُو ٱلْعَرْشِ يُلْقِى ٱلرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ لِيُنذِرَ يَوْمَ ٱلتَّلَاقِ 15
{15} Kisha akataja katika utukufu wake na ukamilifu wake unaohitaji kwamba akusudiwe Yeye tu katika ibada, akasema: "Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye Kiti cha Enzi." Aliyeinuka juu ya Kiti chake cha Enzi, ambacho ni chake peke yake, na ambaye aliinuka juu katika vyeo vyake ambavyo kwavyo alijitenga mbali na viumbe vyake, na ni mwenye sifa tukufu, na ambaye dhati yake ilitukuza kiasi kwamba haiwezekani kujikurubisha kwake isipokuwa kwa matendo matakatifu na safi, ambayo ni ikhlasi inayoinua wenyewe viwango mbalimbali na inawaleta karibu naye na kuwaweka juu ya viumbe vyake vyote. Kisha akataja neema yake juu ya waja wake; kuwatumia wajumbe na ufunuo, akasema: "Hutuma Roho," yaani, ufunuo ambao kwa nafsi na nyoyo ni kama roho zilivyo kwa miili. Kama vile mwili bila roho hauwi hai wala hauishi, basi vile vile nafsi na moyo bila roho ya ufunuo haviwezi kutengenea wala kufaulu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu "hutuma Roho kwa amri yake" ambayo ndani yake yamo manufaa na masilahi kwa waja wake "juu ya amtakaye katika waja wake," ambao ni Mitume wake aliowaboresha na akawateuwa kwa ajili ya kufikisha ufunuo wake na kuwalingania waja kwake. Faida ya kuwatuma Mitume ni kuwafikishia waja furaha yao katika dini yao, dunia yao na akhera yao, na kuwaondolea mambo ya kuwatia mashakani katika dini yao, dunia yao na Akhera yao. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema: "Ili kuonya" waja kutokana na "Siku ya Mkutano" na kuwahofisha na kuwahimiza juu ya kujitayarisha kwa kufanya visababu vya kuwaokoa kutokana na yatakayotokea humo. Aliita Siku ya Mkutano kwa sababu ni siku hii ambapo Muumba na viumbe watakutana, na viumbe wanakutana wao kwa wao, na watendaji matendo na matendo yao na malipo yao.