سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورت 4

An-Nisaa

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 84

فَقَـٰتِلْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفْسَكَ ۚ وَحَرِّضِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۚ وَٱللَّهُ أَشَدُّ بَأْسًا وَأَشَدُّ تَنكِيلًا 84

{84} Hali hii ndiyo hali bora zaidi kwa mja. Kwamba ajitahidi katika nafsi yake kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu ya Jihadi na mambo mengine, na kuwahimiza wengine juu yake. Na mja huenda asiweze kutekeleza amri hizi mbili zote au mojawapo. Ndiyo maana [Mwenyezi Mungu] akamwambia Mtume wake, “Basi pigana vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hutwikwi isipokuwa nafsi yako tu.” Yani huna uwezo juu ya asiyekuwa wewe mwenyewe, na hutatwikwa kufanya kitendo cha asiyekuwa wewe. “Na wahimize Waumini” juu ya kupigana vita. Na hili linajumuisha kila jambo ambalo kwalo Waumini wanapata ukakamavu, na nguvu katika nyoyo zao kama vile kuwatia nguvu, na kujulisha juu ya udhaifu na maadui na kushindwa kwao, na yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia wapiganaji miongoni mwa thawabu, na yale yaliyo juu ya wanaosalia nyuma miongoni mwa adhabu. Basi haya na mfano wake, yote yanaingia katika kuhimiza juu ya kupigana vita. “Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulizi ya wale waliokufuru.” Yani kwa kupigana kwenu katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuhimizana nyinyi kwa nyinyi. “Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia,” yani mkali wa nguvu na utukufu, “na Mkali zaidi wa kutesa” kwa mwenye dhambi katika nafsi yake, na adhabu kwa mwengineye. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, angewashinda makafiri kwa nguvu zake, wala asingewaruhusu abaki yeyote. Lakini kwa sababu ya hekima yake, anawajaribu waja wake wenyewe kwa wenyewe, ili Jihadi isimame imara, na imani yenye manufaa ipatikane, imani ya kuchagua, si imani ya lazima, na ukandamizaji usiofaidi kitu.