سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورت 4

An-Nisaa

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 51

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ نَصِيبًا مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ يُؤْمِنُونَ بِٱلْجِبْتِ وَٱلطَّـٰغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هَـٰٓؤُلَآءِ أَهْدَىٰ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ سَبِيلًا 51

{51} Na haya ni miongoni mwa mabaya ya Mayahudi na husda yao kwa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na Waumini, kwamba tabia zao mbaya na maumbile yao maovu yaliwafanya waache kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na badala yake wakaweka kuamini Al-Jibt na Twaghut. Nao ni kuamini kila ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu au kuhukumu kwa isiyokuwa sheria ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo ikaingia katika hilo uchawi, na ukuhani, na kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kumtii Shetani, vyote hivyo ni katika Jibt na Twaghut. Na vile vile ukafiri na uhasidi viliwapelekea kupendelea njia ya wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu wanaoyaabudu masanamu kuliko njia ya Waumini. Akasema, "Na wanasema kuhusu wale waliokufuru," yani kwa ajili yao. Kwa ajili ya kujipendekeza, na kujilainisha kwao na kwa sababu ya kuichukia Imani, "hawa ndio walioongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini." Basi ni dharau kubwa ilioje, na ukaidi wao mkubwa ulioje, na uchache mno wa akili ulioje? Vipi walichukua njia hii mbaya, na bonde la kulaumiwa? Je, walifikiri kwamba jambo hili litakuwa zuri kwa yeyote kati ya wenye akili au kuingia akilini mwa yeyote katika wajinga? Je, inaweza kuboreshwa dini ambayo imesimama juu ya kuyaabudu masanamu na waabudiwa wengineo, na ikaimarika juu ya kuharamisha mazuri, na kuruhusu maovu, na kuruhusu mengi miongoni mwa yaliyoharamishwa? Na kusimamisha dhuluma baina ya viumbe, na kumtoshanisha Muumba na viumbe, na kumkufuru Mwenyezi Mungu, na Mitume wake, na Vitabu vyake, juu ya dini iliyosimama juu ya ́kumwabudu Mwingi wa Rehema, na kumpwesha Mwenyezi Mungu kwa siri na kwa waziwazi? Na kukufuru vile vinavyoabudiwa badala yake miongoni mwa vyote vinavyoabudiwa, na wenza, na waongo, na juu ya kuunga matumbo ya uzazi, na kuwafanyia wema viumbe vyote, hata wanyama, na kusimamisha uadilifu? Na kufanya haki baina ya watu, na kuharamisha kila maovu, na dhuluma, na ukweli katika kauli zote na matendo yote? Je, hii si isipokuwa ni katika kupayapaya tu? Na mwenye kauli hii ima ni miongoni mwa wajinga wa watu wote na dhaifu wao zaidi wa akili, au ni miongoni mwa wakubwa wao zaidi katika ukaidi na uasi, na kuisukuma haki. Na huu ndio ukweli.