سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورت 4

An-Nisaa

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 25

وَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ مِنكُمْ طَوْلًا أَن يَنكِحَ ٱلْمُحْصَنَـٰتِ ٱلْمُؤْمِنَـٰتِ فَمِن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُم مِّن فَتَيَـٰتِكُمُ ٱلْمُؤْمِنَـٰتِ ۚ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَـٰنِكُم ۚ بَعْضُكُم مِّنۢ بَعْضٍ ۚ فَٱنكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَءَاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ مُحْصَنَـٰتٍ غَيْرَ مُسَـٰفِحَـٰتٍ وَلَا مُتَّخِذَٰتِ أَخْدَانٍ ۚ فَإِذَآ أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَـٰحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى ٱلْمُحْصَنَـٰتِ مِنَ ٱلْعَذَابِ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِىَ ٱلْعَنَتَ مِنكُمْ ۚ وَأَن تَصْبِرُوا۟ خَيْرٌ لَّكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 25

{25} Yani yule ambaye hawezi kupata mahari ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na akajihofia uzinzi na dhiki nyingi, basi anaruhusiwa kuwaoa vijakazi wanaomilikiwa na Waumini. Na hii ni kulingana na inavyoonekana. Vinginevyo, Mwenyezi Mungu anamjua Muumini wa kweli na yule asiyekuwa hivyo. Kwa hivyo, mambo ya dunia yameegemezwa kwenye mwonekano wa nje wa mambo, nazo hukumu za Akhera zimeegemezwa kwenye yale yaliyomo ndani. "Basi waoeni," yani hao waliomilikiwa "kwa idhini ya watu wao;" yani bwana wake mmoja au zaidi. "Na wape mahari yao kulingana na ada;" yani hata kama ni wajakazi, kama vile mahari inavyopaswa kupewa mwanamke huru, kadhalika ni wajibu kumpa mjakazi, lakini hairuhusiki kuwaoa vijakazi isipokuwa ikiwa wao ni "wanawake wema." Yani wanawake wanaojiepusha na zinaa, "si makahaba" yani wanaozini waziwazi, "wala si mahawara" yani wafanyao urafiki wa kimapenzi kwa siri. Na jumla ya hayo ni kwamba hairuhusiki kwa Mwislamu aliye huru kumuoa mjakazi isipokuwa kwa masharti manne aliyoyataja Mwenyezi Mungu: wawe Waumini, wanaojiepusha na machafu kwa nje na kwa ndani, na kutokuwa na uwezo wa kupata mahari ya kuoa mwanamke huru, na kuhofia zinaa. Basi ikiwa masharti haya yanatimia, anaruhusiwa kuwaoa. Na pamoja na haya, uvumilivu juu ya kutowaoa ndiyo bora zaidi, kwa sababu ya yale yaliyo ndani yake ya kuwatia watoto kwenye utumwa, na kwa sababu ya yale yaliyo ndani yake ya uduni na aibu. Na hili ni ikiwa subira inawezekana. Lakini ikiwa haiwezekani kuwa na subira juu ya haramu isipokuwa kwa kuwaoa, basi hilo linakuwa lazima. Na ndio maana akasema, "Na mkisubiri ndiyo bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Na kauli yake, "Na wanapoolewa," yani wajakazi hao wakiolewa au wakisilimu, basi juu yao itakuwa ni nusu ya kile kilichoko juu ya wanawake waungwana walioolewa "katika adhabu." Na hilo ni katika kile ambacho kinaweza kufanywa kuwa nusu, nako ni kupigwa viboko. Basi inakuwa juu yao mijeledi hamsini. Na ama kupigwa mawe, basi mjakazi hapigwi mawe, kwa sababu hilo haliwezi kufanywa kuwa nusu. Na kwa mujibu wa kauli ya kwanza, ikiwa hawajaolewa, basi hakuna Hadd (adhabu maalumu) juu yao, lakini kuna Ta'azir (adhabu ambayo haikukadiriwa) yenye kuwazuia kufanya uchafu huu. Na kwa mujibu wa kauli ya pili ni kwamba wajakazi ambao si Waislamu wakifanya kitendo kichafu, wao pia wanafanyiwa Ta'azir. Na akahitimisha Aya hii kwa majina haya mawili matukufu: Mwenye kufuta dhambi, na Mwenye kurehemu. Kwa sababu, hukumu hizi ni rehema kwa waja, na ni ukarimu, na wema kwao. Na hakuwawekea mipaka, bali ilipanua kikomo cha upana. Na pengine katika kutajwa kwa kufutiwa dhambi baada ya kutaja adhabu ya hadd ni ishara ya kwamba adhabu za hadd ni kafara ambayo kwayo Mwenyezi Mungu hufuta dhambi za waja wake, kama lilivyokuja hilo katika hadithi. Na hukumu ya mtumwa wa kiume katika Hadd (adhabu maalum) iliyotajwa ni kama hukumu ya mjakazi, kwa sababu hakuna tofauti baina yao.