An-Nisaa
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَمَن يَعْمَلْ سُوٓءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُۥ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ ٱللَّهَ يَجِدِ ٱللَّهَ غَفُورًا رَّحِيمًا 110
{110} Kisha Yeye Mtukufu akasema, “Na anayetenda uovu au akaidhulumu nafsi yake, kisha akaomba kufutiwa dhambi kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.” Yani mwenye kuyafanya maasia na akaingia katika dhambi, kisha akatafuta kufutiwa dhambi kufutiwa kukamilifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambako kunalazimu kukiri dhambi, na kuijutia, na kuiacha, na kuazimia kwamba hatarudia; basi huyu ameshaahidi Yule ambaye havunji ahadi yake kufuta dhambi, na rehema. Kwa hivyo atamfutia dhambi alizofanya, na kumwondolea mapungufu na kasoro zilizotokana na hayo, na kumrudishia matendo mema aliyoyafanya kabla, na kumwezesha katika yale yatakayokuja katika maisha yake ya baadaye, na hataifanya dhambi yake kuwa kizuizi cha mafanikio yake. Kwa sababu alikwisha mfutia dhambi. Na akiyafuta, anafuta yale yanayotokana nayo. Na fahamu kuwa kufanya mabaya kwa ujumla kunajumuisha maasia mengine yote, madogo na makubwa. Na huitwa mabaya kwa sababu humwiya mabaya mwenyewe kwa sababu ya adhabu yake, na kwa sababu hayo yenyewe ni mabaya, siyo mazuri. Na vile vile kujidhulumu kunapokuwa hakujafungiwa, kunajumuisha kujidhulumu kwa kufanya ushirikina au kilicho chini yake. Lakini inapounganishwa moja kati ya hizo na nyingine, kila moja inaweza kufasiriwa kwa namna inayolingana nayo. Kwa hivyo, kunafasiriwa kufanya mabaya hapa kwa dhuluma ambayo inawadhuru watu, ambayo ni dhulma katika damu zao, na mali zao, na heshima zao, na inafasiriwa dhuluma kwa nafsi kwa dhuluma na maasia ambayo kati ya Mwenyezi Mungu na mja wake. Na dhuluma kwa nafsi inaitwa dhuluma kwa sababu nafsi ya mja si miliki yake anayoweza kuiendesha atakavyo. Bali ni miliki ya Mwenyezi Mungu, ameiweka kama amana kwa mja, na akamwamrisha kuisimamisha katika njia ya uadilifu kwa kuilazimisha njia iliyonyooka katika elimu na vitendo. Basi anajitahidi kuifundisha aliyoamrishwa, na anajitahidi katika kufanya yale ambayo ni wajibu. Kwa hivyo kufanya kwake juhudi katika isiyokuwa njia hii, ni kuidhulumu nafsi yake, na hiyana, na kuitoa katika matendo ambayo kinyume chake ni ukandamizaji na dhulma.