Az-Zumar
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
قُلْ يَـٰعِبَادِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمْ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ فِى هَـٰذِهِ ٱلدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۗ وَأَرْضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى ٱلصَّـٰبِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ 10
{10} Yaani, sema, ukiwaita watukufu zaidi katika viumbe vyote, ambao ni Waumini, ukiwaamrisha kwa amri iliyo bora zaidi, ambayo ni ucha Mungu, ukiwakumbusha sababu inayowalazimu kuwa wacha Mungu, ambayo ni Umola wa Mwenyezi Mungu juu yao, na neema zake ziwe juu yao kama vile neema ya imani. Hiyo inamlazimu mtu kuwa mcha Mungu, kama unavyoweza kusema: 'Ewe mkarimu, toa sadaka! Ewe shujaa, pigana vita.' Na akawatajia malipo ya kuwatia nasati katika dunia, akasema: "Wale wafanyao wema katika dunia hii" kwa kumuabudu Mola wao Mlezi watapata "wema" kama vile riziki kunjufu, nafsi iliyotulia na moyo mchangamfu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema." "Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu." Mkizuiliwa kumwabudu katika nchi moja, basi hamieni nchi nyingine ambapo mtaweza kumuabudu Mola wenu na kusimamisha Dini yenu. Na pale aliposema: "Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema," watu wengine walikuwa na dhana fulani, maana yake ambayo ni kwamba maneno haya ni ya jumla kwa njia ya kwamba kila atendaye mazuri, atapata mema katika dunia hii. Basi vipi kuhusu mtu anayeamini na anaishi katika nchi ambayo anakandamizwa na kuteswa (kiasi kwamba anashindwa kufanya mazuri), je, hatapata hayo? Kwa hivyo, akaiondoa dhana hii kwa kauli yake: "Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu." Hapa pia kuna bishara njema aliyoisema Mtume, rehema na amani zimshukie, kwamba: "Kundi katika umma wangu litaendelea kushikamana na haki, huku wakiwa washindi, na hatawadhuru wenye kutaka kuwaangusha wala wenye kuwahalifu mpaka itakapofika amri ya Mwenyezi Mungu, nao wako hivyo." Aya hii inalizungumzia hilo na kulirejea kwa njia ya karibu, ambayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kwamba ardhi yake ni pana. Kwa hivyo, hata kama mtazuiliwa kiasi gani kumwabudu katika mahali fulani, basi hamieni kwingine. Hili ni la jumla katika nyakati zote na mahali pote. Kila mhamiaji lazima atapata kimbilio kwa Waislamu ambapo ataweza kukimbilia, na mahali ambapo ataweza kuisimamisha dini yake. "Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hesabu." Hili ni la jumla katika kila aina ya subira: kuwa na subira juu ya mipango michungu ya Mwenyezi Mungu; basi hafai kukasirika kwa sababu yake, kuwa na subira juu ya kutomuasi na kuwa na subira katika kumtii; mpaka akatekeleza utiifu apaswavyo. Kwa hivyo ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa waliosubiri ni kwamba atawalipa bila ya hesabu, yaani bila kikomo, wala kipimo, na hilo si isipokuwa kwa sababu ya ubora wa kuwa na subira na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwamba inasaidia juu ya kila jambo.