Ar-Room
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَهُوَ ٱلَّذِى يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ۚ وَلَهُ ٱلْمَثَلُ ٱلْأَعْلَىٰ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ 27
{27} "Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyingine." Yaani, kuumba viumbe upya baada ya kufa kwao, "ni jepesi zaidi kwake" kuliko kuanzisha kuwaumba. Na hili ni kulingana na bongo na akili. Kwani ikiwa Yeye ni muweza wa kuanzisha ambako nyinyi mnakiri hilo, basi ana uwezo wa kurudisha, ambako ni rahisi zaidi na kunakofailia zaidi kuaminiwa. Na alipotaja baadhi ya ishara zake kubwa ambazo kwazo wenye kuzingatia wanazingatia, na Waumini wanakumbuka, na wanapata ufahamu wale walioongoka, akataja amri kubwa na mahitaji makubwa, akasema, "Naye ndiye mwenye mfano bora zaidi katika mbingu na ardhi." Na huo (mfano bora zaidi) ni kila sifa yenye ukamilifu, na ukamilifu unatokana na sifa hiyo, na mapenzi kamili na toba na kurudi kwake kikamilifu ambako kutoka katika nyoyo za waja wake wanaomkusudia yeye tu, na wanamtaja kwa wingi na wakamuabudu. Mfano bora zaidi ndio maelezo yake ya juu kabisa na yale yanayoambatana na hilo. Na ndiyo maana watu wenye elimu walikuwa wakitumia ulinganisho unaofailia zaidi kuhusiana na Muumba. Walikuwa wakisema: kila sifa ya ukamilifu iliyo katika viumbe; basi Muumba wake ndiye anayestahiki zaidi kusifika nayo kwa namna ambayo hakuna yeyote anayeshiriki naye ndani yake. Na kila upungufu ulio katika kiumbe ambao kinawekwa mbali, basi kumuweka Muumba mbali nao kunafailia na kustahili zaidi. "Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yaani, ana nguvu kamili na hekima pana, na kwa nguvu zake, aliumba viumbe na akadhihirisha maamrisho, na kwa hekima yake, akaumba sawasawa vile alivyounda na akafanya vizuri aliyafanya kuwa katika sheria.