Al-Qasas
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
أَفَمَن وَعَدْنَـٰهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَـٰقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَـٰهُ مَتَـٰعَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ 61
{61} Na kwa sababu hiyo, akazitahadharisha akili kusawazisha baina ya athari za dunia na athari za akhera. Kwa hivyo akasema: "Je, yule tuliyemuahidi ahadi nzuri, tena naye akayapata." Yaani, je, Muumini anayefuta Akhera kwa udi na uvumba, ambaye amefanya kazi kwa ahadi ya Mola wake juu ya malipo mema; ambayo ni Pepo na neema yake kubwa; basi atakutana nayo bila shaka yoyote; kwa sababu ni ahadi kutoka kwa ahadi ya Mkarimu na ya Mkweli ambaye haivunji ahadi ya mtumishi ambaye ametimiza yale yanayomridhisha wake na akaweka kando yale yanayomkasirisha; "ni kama tuliyemstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani." Yeye huchukua ndani yake na hutoa, maumbo na vinywaji, na anafurahia kama wanyama, amejishughulisha na dunia yake badala ya Akhera yake, na hakuinua kichwa kwa mwongozo wa Mwenyezi Mungu, na akawa mkaidi kwa Mitume; na akaendelea vivyo hivyo na maisha hayo, na yakawa malipo ya maisha yake si isipokuwa hasara na kuangamizwa. "Na kisha Siku ya Qiyama akawa miongoni mwa wanaohudhurishwa" kwa ajili ya hesabu. Na hakika anajua ya kwamba hakujifanyia mema, lakini badala yake alijifanyia yote yanayomdhuru, na akahamia kwenye Nyumba ya [thawabu ya matendo]. Basi je, unafikiri nini kitatokea kwake? Na unafikiri atayafanyiwa nini? Hebu mtu mwenye hekima ajichagulie mwenyewe kile ambacho ni bora na kinachostahili zaidi kati ya mambo haya mawili.