سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ash-Shu'araa
سورت 26

Ash-Shu'araa

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیات 57–59

فَأَخْرَجْنَـٰهُم مِّن جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ 57 وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ 58 كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَـٰهَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ 59

{57-59} Kwa hivyo Firauni na askari wake wakatoka nje katika jeshi kubwa na watu wote, na hakuna aliyesalia nyuma miongoni mwao isipokuwa wenye udhuru tu wasioweza kutoka. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Basi tukawatoa katika mabustani na chemchemi;" yaani, bustani za Misri za kifahari na mito inayotiririka na mimea iliyojaa katika ardhi zao na ikaimarishwa kwayo miji yao na vijiji vyao. "Na vyeo vya heshima" ambavyo watazamaji wanapendezwa navyo na ni pumbao kwa wanaovitafakari. Walivifurahia kwa muda mrefu, na wakakata maisha marefu katika raha zake na matamanio yake pamoja na ukafiri wao, ukaidi wao, na kiburi chao juu ya waja na upotofu mkubwa. "Vivyo hivyo, na tukawarithisha hayo Wana wa Israili," ambao walikuwa watumwa wao hapo awali, na wakawatia katika kazi zao ngumu. Basi ametakasika yule anayempa ufalme amtakaye, na anauondoa kwa amtakaye, na humtukuza umtakaye kwa utiifu wake, na humuangusha umtakaye kwa maasia yake.