Ash-Shu'araa
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
قَالَ فَعَلْتُهَآ إِذًا وَأَنَا۠ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ 20 فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِى رَبِّى حُكْمًا وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ 21 وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَىَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ 22
{20-22} Musa akasema, "Nilitenda hayo hapo nilipokuwa miongoni mwa wale waliopotea" na wala si kwamba nilikuwa kafiri. Lakini ilikuwa kwa sababu ya upotofu na upumbavu. Kwa hivyo nikamwomba Mola wangu Mlezi anisamehe, naye akanisamehe. "Basi nikawakimbia nilipowahofu" mliposhauriana kuhusu kuniua, lakini nikakimbilia Madyan, na nikakaa huko kwa miaka, kisha nikawajia ilhali amenitunuku, "hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume." Na jumla ya hayo ni kwamba pingamizi la Firauni kwa Musa ni pingamizi la mjinga au mpumbavu. Alifanya cha kumzuia Musa kuwa Mtume ati ni kule kumuua mtu alikofanya. Kwa hivyo Musa akamweleza kuwa alimuua kwa njia ya upotofu na makosa, na wala hakukusudia kumuua, na kwamba mtu yeyote hawezi kuzuiliwa fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi kwa nini mlizuia kile ambacho Mwenyezi Mungu alinipa cha hukumu na utume? Na anabakia kwako, ewe Firauni, kunibeza kwako kwa kauli yake, "Je, sisi hatukukulea wewe utotoni." Na baada ya uchunguzi mzuri, inabainika kwamba huna neema yoyote uliyotufanyia katika hilo. Na ndiyo sababu Musa akasema, "Na hiyo ndiyo neema" ya kunisumbulia, "na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili?" Nami ukanisalimisha kutokana na kunifanya kuwa mtumwa, na kunitisha, basi ndiyo ukaona kwamba ulinineemesha. Lakini kwa kuangalia vyema, inakubainikia kwamba uhakika ni kuwa uliwadhulumu watu hawa walio bora, na ukawatesa na kuwatiisha kwa kazi zako, nami Mwenyezi Mungu akaniweka salama kutokana na maudhi yako hayo, lakini ukawafikishia kaumu yangu maudhi. Basi ni neema gani hii unayonibeza kwayo?