سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Noor
سورت 24

An-Noor

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 32

وَأَنكِحُوا۟ ٱلْأَيَـٰمَىٰ مِنكُمْ وَٱلصَّـٰلِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَآئِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا۟ فُقَرَآءَ يُغْنِهِمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ 32

{32} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha wasimamizi na mabwana kuwaozesha wale ambao, wako chini ya uangalizi wao kutokamana na masiku, na hali ya kuwa hawana wanaume wala wanawake wakuu na wanawali, basi inampasa yule wa karibu na msimamizi wa yatima kumuozesha anayehitaji kuoa kwa yule kinachomlazimu chakula chake juu yake. Na ikiwa wameamrishwa kumuozesha aliye chini ya mikono yao; basi itakuwa amri yao ya kuoana wenyewe kwa wenyewe ni katika njia iliyokuwa bora zaidi, ''na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu.'' Inawezekana kwamba kinachokusudiwa na mwenye haki ni Swalah al-Din, na kwamba mwadilifu miongoni mwa watumwa wa kiume na wa kike - ambaye si mzinifu, - ameamrishwa na bwana wake kumuoa kama malipo ya uadilifu wake na kumtia moyo kufanya hivyo, na kwa sababu mwovu wa zinaa ni haramu kumwoa, hivyo inaunga mkono yale yaliyotajwa mwanzoni mwa surah kuwa ndoa ya mzinifu na mzinifu ni haramu mpaka atubie, na ateuliwe kwa haki kati ya watumwa na wajakazi kuliko watu huru. Kwa sababu hii ni kawaida kupatikana kwa watumwa. Inawezekana kwamba kile kinachomaanishwa na watu wema katika kuoa na wenye kuhitajia hiyo ndoa kutokamana na watumwa na vijakazi, na haya maana yanaunga mkono ya kwamba Bwana hajaamrishwa kumuoa mtumwa wake kabla ya kumuhitajia kumuoa, na wala matakwa ya maana hayo mawili hayawi mbali kwa wote wawili. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi. Na kauli yake, "ikiwa mafakiri;" yaani, wanaume na wenye kutaka ndoa, ''Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake.'' Kwa hivyo kisiwazuie kile mnachofikiria kwamba atakapooa, atafukarika kwa sababu ya familia yake kubwa na mfano wake. Na ndani yake kuna msisitizo wa kuoa na ahadi kwa mwanandoa kupata utajiri baada ya ufukara. ''Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa,'' mwingi wa kheri na mwenye fadhla kubwa. ''Mwenye kujua;'' kwa Yeyote anayestahili fadhila yake ya kidini na ya kidunia, au mmoja wao ambaye hastahili au mmoja wao asiyestahiki, na humpa kila mmoja wao anachojua na hekima yake inavyohitaji.