An-Noor
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
ٱلزَّانِى لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَٱلزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَآ إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ 3
{3} Haya ni maelezo yanayobainisha uovu wa zinaa, na kwamba huchafua heshima ya mwenye kuitenda, na heshima ya mwenye kuilinganisha na kuichanganya kwa namna ambayo madhambi mengine hayafanyi. Kwa hivyo, akaeleza kwamba mzinifu haoi mwanamke yeyote isipokuwa mwanamke mzinifu, ambaye hali yake na hali ya mwanamke huyo zinanasibiana na kuingiliana, au mshirikina kwa Mwenyezi Mungu ambaye haamini ufufuo wala malipo, wala hajilazimishi katika kufuata amri ya Mwenyezi Mungu. Na mwanamke mzinifu vilevile, hamwoi isipokuwa mwanamume mzinifu au mshirikina. "Na hayo yameharamishwa kwa Waumini." Yaani, imeharamishwa kwao kuolewa na mwanamume mzinifu au kuoa mwanamke mzinifu. Maana ya Aya hii ni kwamba yeyote yule ambaye amesifika na uzinifu, awe mwanamume au mwanamke, na asitubie kwa hilo. Basi yule anayemtanguliza kumwoa, pamoja na kuwa Mwenyezi Mungu ameharamisha hilo haepukiki ima kuwa hashikamani na hukumu za Mwenyezi Mungu na mtume wake na huyo hawi isipokuwa mshirikina, na ima awe ameshikamana na hukumu za Mwenyezi Mungu na mtume wake. Kwa hivyo, akaendelea kumwoa, akijua uzinzi wake; basi ndoa hii ni uzinzi, na ndoa ya mzinifu ni uchafu; ikiwa yeye ni muumini wa kweli wa Mwenyezi Mungu, hawezi kufanya hivo. Na hii ni dalili ya wazi ya kuharamishwa ndoa ya mwanamke mzinifu mpaka atubie. Vile vile, ndoa ya mwanamume mzinifu mpaka atubie. Na hakika kumlinganisha mume na mke wake, na mke kwa mumewe ni ulinganisho mkali zaidi wa uwili, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, “Wakusanyeni waliodhulumu na wake zao;” yaani, wenzao. Basi Mwenyezi Mungu akakataza hilo kwa sababu ya ubaya mkubwa uliomo ndani yake, na uchache wa kuwa na ghera na kuhusisha watoto ambao sio kutoka kwa mume, na kwa kuwa mzinifu hamwachi kwa sababu ya kujishughulisha na mtu mwingine; ambayo baadhi yake ni ya kutosha katika kukataza. Na kwa hili ni dalili ya kwamba mzinifu si muumini, kama alivyosema Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, “Hazini mzinifu wakati anapozini hali yeye ni muumini.” Na yeye hata kama si mshirikina, basi haitiwi kwa jina lenye sifa, ambayo ni imani kamili.