سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
سورت 21

Al-Anbiyaa

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیات 7–9

وَمَآ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۖ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ 7 وَمَا جَعَلْنَـٰهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ ٱلطَّعَامَ وَمَا كَانُوا۟ خَـٰلِدِينَ 8 ثُمَّ صَدَقْنَـٰهُمُ ٱلْوَعْدَ فَأَنجَيْنَـٰهُمْ وَمَن نَّشَآءُ وَأَهْلَكْنَا ٱلْمُسْرِفِينَ 9

{7-9} Hili ni jibu kwa mfano wa wale wanaomkanusha mtume wanaosema: Je, (kwa nini) asingekuwa malaika asiyehitaji chakula na kinywaji na kutenda katika masoko?" Kwa nini asingekuwa mwenye kuishi milele (asiyekufa)! Ikiwa sivyo, inaonyesha kwamba yeye si mjumbe! Ulinganifu huu bado uko katika nyoyo za wale wanaowakanusha Mitume, ambao wanafanana katika ukafiri; kwa hivyo kauli zao zikafanana. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu alijibu mfanano huu, kwa wale wanaowakanusha Mitume, wanaokiri kuthibiti kwa Mitume kabla yake, hata lau kama hakuwa ispokuwa Ibrahim amani iwe juu yake, ambaye wamekiri unabii wake kwa madhehebu yote, na washirikina wanadai kwamba wako kwenye dini na madhehebu yake. Kwamba Mitume kabla ya Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu iwe juu yake - wote ni wanadamu wanaokula chakula na kutembea sokoni, na dalili za kibinadamu zinatokea kwao kutoka kwa kifo na mengineyo, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa watu wao na umma wao. Kwa hivyo waliaminiwa na wale waliowaamini, na wakakanushwa na wale waliowakanusha, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwasadikisha kile alichowaahidi kutokamana na wokovu na furaha kwao na wafuasi wao, na akawaangamiza wabadhirifu na wakanushaji wao. Na je, vipi kuhusu Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - unasimamishwa mfanano wa uovu juu ya kupingwa utume wake, nalo ni jambo lenye kupatikana kwa ndugu zake wajumbe, ambao wakanushaji wanawakurubisha zaidi kwa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake? Huu ni wajibu ulio wazi kwao, na ikiwa wanakiri mjumbe wa kibinadamu, na wasimkubali mjumbe asiye wa kibinadamu, kwamba mfano wao ni batili, wameubatilisha kwa kukiri upotovu wake na kuupinga. Na lau kuwa ingechukuliwa kugeuka kwao huku hadi kupinga unabii wa mwanadamu moja kwa moja, na kwamba hawezi kuwa nabii ikiwa yeye si malaika asiyeweza kufa, ambaye hali chakula. Basi hakika Mwenyezi Mungu tayari alishajibu itikadi hii potofu kwa kauli yake, "Na walisema, 'Mbona hakuteremshiwa Malaika?' Na kama tungelimteremsha Malaika, basi bila ya shaka jambo hilo lingelikwisha hukumiwa, kisha wasingelipewa muhula. Na kama tungelimfanya Malaika, bila ya shaka tungelimfanya kuwa mwanamume, na tungeliwatilia matatizo yale wanayoyatatiza wao." Na kwamba wanadamu hawana uwezo wa kupokea ufunuo kutoka kwa malaika. "Sema: Ingelikuwa katika ardhi wapo Malaika wanaotembea kwa utulivu, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao." Na kama mna shaka na mkakosa kujua hali ya Mitume waliotangulia, basi waulizeni wenye elimu katika watu wa vitabu vilivyotangulia, kama vile watu wa Taurati na Injili, wawaambie yale waliyo nayo katika elimu, na kwamba (Mitume hao) wote walikuwa wanadamu wa aina sawa na wale waliotumwa kwao. Na aya hii, hata kama sababu yake ni mahususi katika kuuliza juu ya hadhi ya Mitume waliotangulia miongoni mwa watu wa ukumbusho, ambao ni watu wa elimu, lakini ni ya jumla katika kila suala miongoni mwa masuala ya Dini: misingi yake na matawi yake, ikiwa mtu hana elimu kuhusiana nayo kwamba amuulize yule anayeyajua. Basi ndani yake kunayo amri ya kujifunza na kuwauliza watu wa elimu. Na haikuamrishwa kuwauliza isipokuwa kwa sababu ni wajibu juu yao kufundisha na kujibu yale wanayoyajua. Na katika kufanya suala la kuwauliza Watu wa ukumbusho na wenye elimu kwamba ni mahususi na hawa tu, kuna katazo la kumuuliza anayejulikana vyema kwamba ni mjinga asiyekuwa na elimu, naye pia amekatazwa kujipeleka mbele katika kujishughulisha na hili. Na katika aya hii, kuna ushahidi kwamba hakuna nabii yeyote wa kike aliyewahi kutokea, si Maryamu wala mtu mwingine yeyote, kwa sababu ya kauli yake, "isipokuwa wanaume."