Taa-Haa
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَقَالُوا۟ لَوْلَا يَأْتِينَا بِـَٔايَةٍ مِّن رَّبِّهِۦٓ ۚ أَوَلَمْ تَأْتِهِم بَيِّنَةُ مَا فِى ٱلصُّحُفِ ٱلْأُولَىٰ 133
{133} Wale wanaokadhibisha walimwambia Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, 'Kwa nini hatuletei Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?' Wakimaanisha ishara wanazozipendekeza wao, kama vile kauli yao, "Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchemi katika ardhi hii. Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai; au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso.” Huu ni usugu, ukaidi na dhuluma kwa upande wao. Kwa maana, wao na Mtume ni watu, waja wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, haiwafailii kupendekeza kwa matamanio yao, bali mwenye kuiteremsha na akachagua kutoka humo anachokichagua kwa hekima yake ni Mwenyezi Mungu. Na kwa kauli yao: ''Lau asingalituletea Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi;'' ina maana kwamba hakuwaletea dalili ya ukweli wake wala ushahidi wa ukweli wake, na huu ni uongo na kashfa kwani ameleta miujiza ya kung'aa na dalili zinazotekeleza baadhi ya yale yaliyokusudiwa. Na ndiyo maana akasema: ''Je, haujawajia ikiwa kweli wao ni wakweli katika yale wanayoyasema, na wakatafuta haki kwa ushahidi wake, ''Ushahidi ulio wazi wa yaliyomo katika kurasa za mwanzo?'' Qur-ani hii kubwa inayosadikisha yale yaliyomo katika kurasa za kwanza za Taurati, Injili, na vitabu vilivyotangulia, vinawiana navyo, vinafahamisha yale waliyoambiwa, na uthibitisho wake pia umetajwa ndani yake. Na anabashiria Mtume wake, na hii ni kama kauli yake Mwenyezi: ''Je, haikutosha kwao kuwa tumekuteremshia Kitabu ili wasomewe? Hiyo ni rehema na mawaidha kwa watu wanaoamini.'' Aya zinawanufaisha Waumini na zinawazidishia Imani na yakini, lakini wanaojiepusha nazo ni wale wanaowapinga. Hawaiamini na wala hawafaidiki nayo. "Hakika wale ambao neno la Mola wako limekwisha thibitika juu yao hawataamini." "Ijapokuwa itawajia kila Ishara, mpaka waione adhabu chungu."