Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
فَأَزَلَّهُمَا ٱلشَّيْطَـٰنُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا ٱهْبِطُوا۟ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَـٰعٌ إِلَىٰ حِينٍ 36
(36) Basi wakadanganyika naye na wakamtii. Hivyo basi, akawatoa katika yale waliyokuwamo katika neema na ukunjufu; na wakashukishwa kwenda katika nyumba ya taabu, uchovu na kupambana. “Nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi.” Yani Adam na kizazi chake ni maadui wa Iblis na kizazi chake. Na kama inavyojulikana, adui hukakamia na kujitahidi katika kumdhuru adui yake na kumfikishia shari kwa kila njia, na kumnyima heri kwa kila njia. Hivyo basi, ndani ya haya kuna tahadharisho kwa wanaadamu dhidi ya Shetani, kama alivyosema (Mwenyezi Mungu) Mtukufu: “Hakika Shet'ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni.” “Je, Mnamfanya yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.” Kisha akataja mwisho wa kuteremka katika ardhi, akasema: “Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu,” yani maskani na mahali pa kutua “na starehe kwa muda.” Wa kwisha kwa muda wenu, kisha mtatoka humo kwenda kwenye nyumba ambayo mliumbwa kwa ajili yake, nayo ikaumbwa kwa ajili yenu. Na katika aya hii kuna kwamba muda wa maisha haya (ya duniani) ni ya muda mfupi na wa kupita, siyo maskani ya kweli. Lakini, ni njia ya mapito ambayo mtu anapaswa kuchukua chakula kutoka humo kwa ajili ya nyumba ile nyingine, na wala haifai kuyaimarisha kwa ajili ya kukaa humo milele.