سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورت 2

Al-Baqara

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 30

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى جَاعِلٌ فِى ٱلْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوٓا۟ أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّىٓ أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ 30

(30) Huu ni mwanzo wa kutaja uumbaji wa Adam, amani iwe juu yake, baba wa wanadamu na fadhila zake, na kwamba Mwenyezi Mungu alipotaka kumuumba; aliwaambia Malaika hayo, na kwamba Mwenyezi Mungu atamfamya kuwa Khalifa (mfwatizi) katika dunia. Malaika amani iwe juu yao wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo kwa maasia na kumwaga damu. Na huku ni kutaja kilicho maalum baada kutaja cha jumla, ili kubainisha ukubwa wa uharibifu wa kuua. Na hii ni kwa mujibu wa dhana (fikra) zao kwamba huyo Khalifa atakayewekwa katika ardhi atayafanya hayo. Kwa hivyo wakamtakasa Al-Bari (Mola Muumbaji) kutokana na hilo, na wakamtukuza, na wakamwambia kwamba wao kwa hakika wanamuabudu Mwenyezi Mungu kwa njia ambayo haina uharibifu, wakasema: “Hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako.” Yani tunakutakasa utakaso unaolingana na sifa zako na utukufu wako, “na tunakutaja kwa utakatifu wako?” Maana yake inaweza kuwa: Tunakutakasa Wewe. Basi inakuwa herufi Laam hapo ni yenye maana ya kumteua na kumpwekesha Mwenyezi Mungu peke yake katika hilo. Na inaweza kuwa na maana; “na tunakutakasia Wewe nafsi zetu.” Yani tunazisafisha kwa tabia nzuri kama vile kumpenda Mwenyezi Mungu, na kumnyenyekea, na kumtukuza. Na tunazitakasa kutokana na maadili maovu. “Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kuwaambia Malaika: “Hakika Mimi nayajua” kuhusu huyu khalifa “msiyoyajua” Kwa sababu maneno yenu ni kulingana na dhana (fikira) yenu, nami ninajua (mambo) ya siri na ya dhahiri. Na ninajua kwamba heri itakayotokea kwa kumuumba huyu khalifa inazidi kwa mizidisho mingi kilichomo ndani yake cha uovu. Na kama haingekuwa katika hili isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu alitaka kuteua kati yao Manabii, Masidiqi (wakweli), Mashahidi, na watu wema, na ili awadhihirishie vuimbe ishara zake. Na ili zifanyike ibada ambazo hazingefanyika bila ya kumuumba huyu khalifa, kama vile jihadi na mengineyo. Na ili afichue yaliyofichika katika silika ya wanadamu ya kheri na shari kwa kuwafanyia mtihani, na ili adhihirike adui wake na rafiki wake, na kikundi chake kutokana na wanaompiga vita, na ili yadhihirike yaliyofichika katika nafsi ya Iblisi ya shari iliyomfunika, na akasifika kwayo, basi hizi ni hekima kubwa, baadhi yake inatosha katika hilo.