Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
يُؤْتِى ٱلْحِكْمَةَ مَن يَشَآءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ ٱلْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِىَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ 269
{269} Alipotaja hali za watoao mali, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwapa na akawaneemesha na mali ambazo wanazitoa katika njia za heri. Na wanapata kwazo daraja tukufu, akataja kilicho bora kuliko hayo. Nacho ni kwamba yeye humpa hekima amtakaye katika waja wake, na anayewatakia heri katika viumbe vyake. Na hekima ni elimu zenye manufaa, na maarifa sahihi, na akili zilizonyooka, na uelewa timamu, na kufikia usahihi wa maneno na vitendo. Na hiki ndicho kipawa bora zaidi na zawadi kubwa zaidi. Na ndiyo maana akasema: "Na mwenye kupewa hekima, basi bila ya shaka amepewa heri nyingi." Kwa sababu, alitoka kwenye giza la ujinga hadi kwenye nuru ya uwongofu. Na kutoka katika upumbavu wa kupotoka katika maneno na vitendo hadi kufikia usahihi katika hayo, na kupata kunyooka. Na kwa sababu aliikamilisha nafsi yake kwa heri hii kubwa, na akajitayarisha kuwanufaisha viumbe manufaa makubwa zaidi katika dini yao na dunia yao. Na mambo yote hayawi mazuri isipokuwa kwa hekima ambayo ni kuweka vitu mahali pake, na kuteremsha vitu katika daraja zake. Na kwenda mbele katika pahali pa kwenda mbele, na kurudi nyuma katika pahali pa kurudi nyuma. Lakini halikumbuki jambo hili kubwa, na hajui thamani ya kipawa hiki kikubwa, "isipokuwa wenye ufahamu." Na wao ni wale wenye akili ya kutosha na busara kamilifu. Hao ndio wanaojua chenye manufaa na kwa hivyo wanakifanya. Na chenye madhara, kwa hivyo wanakiacha. Na mambo haya mawili ambayo ni kutoa matumizi ya kimali kwa wingi, na kutoa hekima ya kielimu kwa wingi, ndiyo bora zaidi cha vile wanavyojikurubisha kwavyo wale wanaojikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Na ndiyo ya juu zaidi waliyoyafika kwayo utukufu mkubwa. Na ndiyo mawili aliyoyataja Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwa kauli yake. “Hapana husuda isipokuwa katika mambo mawili: Mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa mali, basi akampa mamlaka juu ya kuitumia katika haki. Na mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa hekima, kwa hivyo huifundisha kwa watu.