Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَقَـٰتِلُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ 244 مَّن ذَا ٱلَّذِى يُقْرِضُ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَـٰعِفَهُۥ لَهُۥٓ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَٱللَّهُ يَقْبِضُ وَيَبْصُۜطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ 245
{244 - 245} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiunganisha pamoja amri ya kupigana vita katika njia yake kwa mali na mwili. Kwa sababu, jihadi haisimami isipokuwa kwa mambo mawili haya. Na alihimiza juu ya kuwa na ikhlasi ndani yake kwamba mja apigane ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu. Kwa maana, kwa hakika Mwenyezi Mungu "ni Mwenye kusikia" maneno hata yakifichika. "Ni mwenye elimu" juu yale yaliyomo ndani ya nyoyo kama vile nia njema na kinyume chake. Pia yule anayefanya jihadi katika njia yake anapojua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye elimu, hilo linamuwiya rahisi. Na anajua kwamba hakika Yeye ni wale wanaovumilia kwa ajili Yake, na kwamba hakuna budi awape msaada na wema wake. Na tafakari kuhimiza huku kupole juu ya kutoa, na kwamba mtoaji huwa amemkopesha Mwenyezi Mungu, Tajiri, Mwingi wa ukarimu. Na akamuahidi mizidisho mingi, kama alivyosema Mola Mtukufu. "Mfano wa wale wanaotumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua." Na kwa vile kizuizi kikubwa kinachozuia kutoa ni kuhofia umasikini, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa utajiri na umasikini vimo mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba Yeye huikunja riziki kwa amtakaye, na huikunjua kwa amtakaye. Basi na asichelewe anayetaka kutoa kwa kuhofia umasikini. Na wala asifikirie kuwa amepoteza, bali marejeo ya waja wote ni kwa Mwenyezi Mungu. Kisha watoaji na watendaji kazi watapata malipo yao kwake; wameekewa akiba watakapokuwa wanayahitaji zaidi. Na hilo litawaathiri vikubwa kiasi ambacho haiwezekani kueleza. Na maana ya mkopo mzuri ni ule unaojumuisha sifa za wema kama vile nia njema na ukunjufu wa nafsi wakati wa kutoa. Na kuifikisha katika mahali pake, na kwamba mtoaji asiufuatishe kwa masimbulizi. Wala udhia, wala kubatilisha na kupunguza.