Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَٰجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ 234
{234} Yani mume atakapokufa, mke wake atakaa akingoja kwa lazima miezi minne na siku kumi. Na hekima katika hilo ni kubainisha mimba katika muda huo wa miezi minne. Naye mtoto aliye ndani ya tumbo ataanza kusongasonga mwanzoni mwa mwezi wa tano. Na ujumla huu umefanywa kuwa mahususi katika hali ya wanawake wajawazito. Hao eda yao inaisha kwa kuzaa. Na vile vile mjakazi, muda wake ni nusu ya muda wa mwanamke huru; miezi miwili na siku tano. Na kauli yake "na wakimaliza muda wao (wa eda), basi hakuna ubaya wowote juu yao katika yale wanayozifanyia nafsi zao." Yani kuyarudia kwao mapambo na manukato "kwa wema" yani namna isiyokuwa haramu wala inayochukiza. Na katika hili kuna ulazima wa kuacha mapambo katika muda wa eda kwa mwanamke aliyefiwa mume peke yake. Siyo wale wanawake wengineo wanaoachwa kwa talaka na kuachana kwingineko. Na hili wamekubaliana juu yake wanachuoni. "Na Mwenyezi Mungu anazo habari zote za mnayoyatenda." Yani anayajua matendo yenu, ya dhahiri yake na ya ndani yake, ya waziwazi kabisa na yaliyofichika, kisha atawalipa juu yake. Na katika kuwaongelesha kwake wasimamizi (wa wanawake) katika kauli yake, "basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika yale wanayozifanyia nafsi zao." Kuna dalili ya kwamba msimamizi amtunze mwanamke na amzuie yale yasiyoruhusiwa kufanywa. Na amlazimishe kufanya yale ambayo ni ya lazima, na kwamba yeye ndiye anayeongeleshwa hayo, na ni wajibu juu yake.