Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ ٱلْبَأْسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلْزِلُوا۟ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ مَتَىٰ نَصْرُ ٱللَّهِ ۗ أَلَآ إِنَّ نَصْرَ ٱللَّهِ قَرِيبٌ 214
Yeye Mwenye baraka na Mtukufu anajulisha kwamba ni lazima awajaribu waja wake kwa yenye wasaa na yenye dhiki na taabu, kama alivyowafanyia wale waliokuwa kabla yao. Kwani hii ndiyo ada yake inayoendelea ambayo haigeuki wala haibadiliki, kwamba mwenye kusimamisha dini yake na sheria yake lazima ajaribiwe. Akisubiri juu ya amri ya Mwenyezi Mungu na hayajali machukizo yanayotokea katika njia yake, basi yeye ndiye mkweli ambaye amepata katika furaha ukamilifu wake, na katika ukuu chombo chake. Na mwenye kufanya mateso ya watu kuwa kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba machukizo yakamzuia yale anayokaribia kuyafanya. Na majaribio yakamzuia lengo lake, basi yeye ndiye mwongo katika madai ya kuwa na imani. Kwani, imani sio kwa kujipamba na kutamani tu, na madai matupu, mpaka matendo yaisadikishe au yaikadhibishe. Na yaliwatokea mataifa ya kale yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu juu yao. “Uliwapata ufukara (shida) na maradhi” katika miili yao “na wakatikiswa” kwa aina mbalimbali za hofu kama vile vitisho vya kuuawa, kuhamishwa, kuchukuliwa mali, kuuawa kwa vipenzi, na aina mbalimbali za madhara mpaka hali ikawafikisha. Na mitetemeko ikawafikisha kuona kwamba nusura ya Mwenyezi Mungu imechelewa pamoja na kuwa na yakini nayo. Lakini kwa sababu ya ukali na jambo hilo, na dhiki yake, alisema: Mtume na walioamini pamoja naye wakasema: “Ni lini nusura ya Mwenyezi Mungu (itakuja?)” Na kwa kuwa faraja huja wakati wa ugumu, na kila jambo linapokuwa finyu, linakunjuka, Mwenyezi Mungu akasema: “Jueni kuwa hakika nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.” Na namna hiyo, kila mwenye kuisimamia haki, yeye kwa hakika atajaribiwa. Na kila inapokuwa hali ni kali na ngumu kwake, ikiwa atadumu na akavumilia katika yale aliyomo ndani yake, basi majaribio yanageuka katika haki yake na yanakuwa neema. Na dhiki zinakuwa raha mbalimbali, na hayo yakamfuatisha ushindi juu ya maadui na uponyaji wa maradhi yaliyomo ndani ya moyo wake. Na Aya hii ni sawa na kauli yake Mola Mtukufu. “Je, mnadhani kwamba mtaingia Peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawapambanua wale miongoni mwenu waliopigana Jihadi, na hajawapambanua waliosubiri?” Na kauli yake Mtukufu: “Je, wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? Hakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.” Na wakati wa mtihani, mtu hupewa heshima au hudunishwa.