Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
أَيَّامًا مَّعْدُودَٰتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى ٱلَّذِينَ يُطِيقُونَهُۥ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُۥ ۚ وَأَن تَصُومُوا۟ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ 184
{184} Na alipotaja kuwa aliwafaradhishia kufunga Saumu, alitoa habari kuwa ni siku zenye kuhesabika, yani chache na rahisi sana. Kisha akafanya urahisi mwingine. Akasema “Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini, basi atimize hesabu katika siku nyingine.” Na hayo ni kwa sababu ya ugumu (dhiki) mara nyingi, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaruhusu wafungue. Na kwa kuwa ilikuwa ni lazima kila Muumini kupata faida ya kufunga Saumu, akawaamrisha walipe katika siku nyingine ugonjwa unapoisha, na safari ikaisha, na raha (kupumzika) ikapatikana. Na katika kauli yake, “basi atimize hesabu katika siku nyingine.” Kuna dalili ya kwamba analipa kwa idadi ya siku za Ramadhani, sawa (mwezi) ulikuwa kamili au mpungufu. Na kwamba inaruhusika kulipa siku zilizokuwa fupi zenye baridi katika siku ndefu zenye joto, na kinyume chake. Na kauli yake “Na wale wanaoweza kufunga” yani wanaoweza kufunga Saumu, “watoe fidia” kwa kila siku wanayofungua ndani yake “kwa kumlisha masikini”. Na hii (hukumu) ilikuwa mwanzoni mwa kufaradhishwa kufunga Saumu, walipokuwa hawajazoea kufunga saumu. Na pindi kuifanya kuwa faradhi juu yao kungekuwa bila shaka na ugumu juu yao, ndio maana Mola Mlezi, Mwenye hekima akawawazoesha kwa njia nyepesi. Na akampa hiari mwenye uwezo wa kufunga Saumu kati ya kufunga Saumu, nalo ndilo bora, au kulisha (masikini). Ndiyo akasema: “Na mkifunga ndiyo bora kwenu.” Kisha baada ya hayo akafanya kufunga Saumu kuwa lazima kwa wale wenye uwezo. Nao wasioweza, wanafuturu na wanazilipa katika siku nyingine. [Na ilisemwa maana yake ni “wale wanaoweza kufunga,” yani wanoweza kwa shida, na kufunga kunawawia kugumu; ugumu ambao haustahimiliki. Kama vile mzee sana, basi atalipa fidia kwa kila siku masikini, na hii ndiyo kauli sahihi].